Kakonko;Vijana wanaomaliza mafunzo awali ya kijeshi katika vikosi vya jeshi la kujenga Taifai hapa nchini wametakiwa kuwa na unyenyekevu na nidham na kufuata taratibu na sheria za nchi wakizingatia mafunzo na maelekezo wanayopewa, ili jamii iweze kupata manufaa ya kuwepo kwa jeshi hilo
Mwemezi MuhingoMwananchi
Kakonko;Vijana wanaomaliza mafunzo awali ya kijeshi katika vikosi vya jeshi la kujenga Taifai hapa nchini wametakiwa kuwa na unyenyekevu na nidham na kufuata taratibu na sheria za nchi wakizingatia mafunzo na maelekezo wanayopewa, ili jamii iweze kupata manufaa ya kuwepo kwa jeshi hilo
Akiwahutubia jana, mamia ya wahitimu wakufunzi , Askali na wananchi wa kawaida wakati wa kufunga mafunzo ya kijeshi kwa vijana mujibu wa sheria Oparation Magufuli Mkuu wa wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma Canol Hosea Ndagala ambae alikuwa mgeni rasmi kikisi 824 Kanembwa amesema kwa kuwa Askali ni Raia daraja la pili hivyo ni lazima kufuata maadili na kinyume chake huyo si Askali
Mkuu wa JKT hapa nchini Brigedia General Michael Isamuyo aliyewakilishwa na Luten Canol Joseph P Mahende aliwambia wahitimu hao kuwa ni mambo mengi waliyojinfunza jeshini ambayo hapo awali hawakuyafahamu walipokuwa mashuleni, hivyo ni vema wakayazingatia kwa ajili ya Faida yao na Taifa kwa ujumla huku Mkuu wa Kikos hicho Luten Canol Amos Molo akieleza kuwa vijana hao wamepata mafuzo katika silabi mbalimbali kulingana na ngazi yao
Awali Katika lisara yao wahitimu hao, iliyosomwa na Karoline Aweso walisema kuwa changamoto ambazo wamekabiliana nazo ni ukosefu Gari la kubeba wagonjwa kikosini hapo hali ambayo inasababisha usumbufu pale anapotokea mgonjwa na kupewa rufaa na kuiomba serikali kukipatia kikosi hicho Gari la kubeba wagonjwa ili kuondoa usumbufu
Ibrahim Bewe, ambaye ni mmoja wa wahitimu aliipongeza serikali kwa uwamuzi wake wa kurejesha tena upya jeshi la kujenga Taifa ambalo lilistishwa miaka iliyopita akieleza kuwa JKT kimekuwa ni kitovu muhimu kwa malezi ya Vijana huku akiwataka vijana wenzake wanaopata nafasi kujiunga na jkt kutozipuuza
Vijana walihitimu mafunzo hayo ya Kijeshi kwa mujibu wa sheria oparation Magufuli, ni wale waliomaliza kidato cha sita mwaka huu na waliobahatika kumaliza katika kikosi cha 824 kj Kanemba JKT ni 11016
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni