Kakonko; Watanzania wametakiwa kujenga tabia ya kulinda mali za umma huku wakitambua kuwa ni kodi za na ni kwa manufaa yao wenyewe hivyo hawana budi kutoa taarifa katika mamlaka husika pale wanapoona kuna dalili za kuhodhiwa au kuhujumiwa kwa mali hizo
Baadhi ya wananchi na wafanyakazi wa halmashauri ta kakonko waliohudhiria utilianaji wa sahihi mkataba ujenzi wa halmashauri hiyo kati yake na kampuni Magaco ya mjini Dodoma |
Kakonko; Watanzania wametakiwa kujenga tabia
ya kulinda mali za umma huku wakitambua kuwa
ni kodi za na ni kwa manufaa yao wenyewe hivyo hawana budi kutoa taarifa
katika mamlaka husika pale wanapoona kuna dalili za kuhodhiwa au kuhujumiwa kwa
mali hizo
Mkurugenzi mtendaji wa
Halmashauri ya wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Lusubiro Joel akizungumza wakati
wa hafla fupi ya kutiliana saini mkataba wa ujenzi wa ofisi za Halmashauri ya
wilaya hiyo na Mkandarasi Magacon Constraction limited ya Mjini Dodoma juzi,
Lusubiro alisema watu wengi ubaki wakilalamika
badala ya kutoa taarifa ili kuzuia uharibifu zaidi huku akiwasisitiza
wananchi kutembelea eneo la ujenzi wa osifi hizo na kuhoji pale wasipoelewa
mambo juu ya mambo yanayoendelea
‘’Tumeamua katika halmashauri yetu kufanya mambo wazi hale
yale yanayotakiwa kuwa wazi kwakuwa tofauti hatua hiyo, kazi au mikataba
inapokwenda tofauti na wananchi waposhirikishwa baada ya mapungufu kuonekana
ndicho chanzo cha jamii kukata hata kujitoa kushirika katika miradi ya
maendeleo tena inayowahusu wao wenye alisema Lusubiro’’
Halmashauri hiyo changa
changa, kwa sasa inatumia majengo ya kuazima kwa ajili ya kuendesha
shughuli zake hali ambayo imekuwa haikidhi mahitaji kwakuwa ofisi zingine ziko
kwenye makazi ya watu kama alivyoeleza Juma Maganga mwenyekiti wa Halmashauri
hiyo huku Mkurugenzi wa Kampuni iliyochukua Kandarasi ya ujenzi huo Philipo
Majani akiahidi kumaliza kwa muda uliopangwa
Ujenzi wa ofisi hizo unatarajia kugarimu kiasi cha shilingi Bilion 2.6 hadi kukamilika na
mkataba wa awali unaolenga sehemu ya ofisi hizo unatarajia kugarimu shilingi
milion 365.
Mkuu wa wilaya hiyo
Canal Hosea Ndagala amemtaka mkadarasi huyo kufanya kazi kwa uadilifu akitambua
kuwa fedha hizo ni nyingi na kuwa ni fedha za walipa kodi, huku mmoja wa
watumishi wa halmashauri ya kakonko Christopha msafiri akieleza shida
wanazokumbana nazo kutoka na uhaba wa vyumba vya kufanyia kazi
Eneo litakalo jengwa ofisi za halmashauri w kakonko |
Philipo Majani mkurugenzi wa kampuni ya Magacon wakipeana mikono na mkurugenzi mtendaji halmashauri ya kakonko Lusubiro Mwakabibi baada ya kusainiana mkataba wa ujensi |
Baadhi ya wananchi
waliohudhulia hafla hiyo ambapo mmoja wao ni Masoud Halfan wamefuhishwa na kitendo cha
kushirikishwa katika zoezi la utiaji saini wakieleza kuwa mambo mengi yamekuwa
yakiendeshwa kimyakimya hatua ambayo isingewezekana kuingilia kati pale mambo
yanapokwenda tofauti kwani wanakuwa hawafahamu kinachoendelea
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni