Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2016

Kibondo;Mkuu wa wilaya ya Kibondo mkoani kigoma Luis Bura amemwagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo kuwasimamisha kazi watumishi 3 wa idara ya ujenzi kutokana na ubadhilifu wa fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba ya walimu katika shule ya sekondari Itaba

Picha
Kibondo; Mkuu wa wilaya ya Kibondo mkoani kigoma Luis Bura amemwagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo kuwasimamisha kazi watumishi 3 wa idara ya ujenzi kutokana na ubadhilifu wa fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba ya walimu katika shule ya sekondari Itaba Watumisha hao wanatuhumiwa kudanganya ili mkandarasi anaejenga nyumba hizo kulipwa milion 109 malipo ya wamu ya pili kwa madai kuwa ujenzi umekemilika kwa asilimi 85% ambapo milion 46 zimelipwa bila kufanyiwa kazi yoyote huku ujenzi ukiwa chini ya viwango na ukiwa uko chini ya asilimia 50% kama alivyoeleza mkurugenzi wa halmashauri hiyo Juma Mlehe kwa waandishi wa habari na wananchi Mkuu huyo wa wilaya katika maelezo yake alisesema matatizo ya ubadhilifu wa fedha za serikali katika wilaya hiyo yamekuwa ni mambo ya kawaida huku akilalamikia makundi ya wanasiasa kuingilia shughuli za kitaalam kwa kuwalazimisha watumishi wa halmashauri kufanya  mambo wanayoyataka wao  na kuwa...

Mgombea wa urais wa Marekani kwa tikiti ya chama cha Republican Donald Trump ameimarisha kampeini zake mjini Nevada licha ya kisa cha usalama kilochobabisha walinzi wake kumuondoa jukwaani kwa muda.

Picha
Mgombea wa urais wa Marekani kwa tikiti ya chama cha Republican Donald Trump ameimarisha kampeini zake mjini Nevada licha ya kisa cha usalama kilochobabisha walinzi wake kumuondoa jukwaani kwa muda. Wafuasi wake wanasema walinzi wake walifanikiwa kumuondoa jukwaani licha ya hofu kwamba kulikuwa na mtu aliyekuwa amejihami kwa silaha miongoni mwao. Bw.Trump alikuwa anakaribia kilele cha hotuba yake ndani ya ukumbi wa Reno uliyojaa wafuasi wake, na ghafla kukatokea rabsha karibu na jukwaa. Taharuki ilitanda mahala hapo kabla ya walinzi wake kufanikiwa kumuondoa. Wafuasi wake waliyojawa na hofu walianza kukimbilia lango la kutoka nje wa ukumbi huo kufuatia madai ambayo hayakudhibitishwa Polisi wamemkamata mtu mmoja kufuatia tukio hilo lakini akaachiliwa muda mfupi baadaye. Mtu huyo hakupatikana na silaha kama ilivyodaiwa. Huku zikiwa zimesalia siku tatu kabla ya uchaguzi mkuu,wagombea wote wawili wameimarisha kampeini zao katika jimbo muhimu la Florida linalo na umaarufu w...

Idadi ya wakimbizi raia wa Burundi wanaoendelea kuikimbia nchi yao kutokana na machafuko ya kisiasa yaliyoanza toka mwezi April mwaka jana nakupewa hifadhi katika kambi ya Nduta iliyopo wilayani Kibondo Mkoani Kigoma imeendelea kuongezeka siku hadi siku.

Idadi ya wakimbizi raia wa Burundi wanaoendelea kuikimbia nchi yao kutokana na machafuko ya kisiasa yaliyoanza toka mwezi April mwaka jana nakupewa hifadhi katika kambi ya Nduta iliyopo wilayani Kibondo Mkoani Kigoma imeendelea kuongezeka siku hadi siku. Hayo ya mebainishwa na mkuu msaidizi wa kambi hiyo Bi Jeska Ntaita alipozungumza na  Clouds fm kuhusiana na idadi ya wakimbizi wanaoendelea kupokelewa kwenye kambi hiyo pamoja na changamoto kwenye kambi hiyo. Amesema hadi sasa kambi hiyo imepokea zaidi ya wakimbizi 55,500 (hamsini natano elfu na miatano) na kwamba changamoto ya maji iliyokuwa ikiikabili kambi hiyo ikiwa inaendelea kushughulikiwa Aidha Bi Ntaita amesema kambi hiyo ilisimama kupokea wakimbizi hao kutokana na hapo awali kuwa natatizo kubwa la uhaba wa maji na sasatatizo la hilo la limeshughulikiwa na sasa wana mpango wakuendelea kuwapokea wakimbizi hao hadi kufikia 60,000 ilikupunguza msongamano kwenye kambi zingine zinazoendelea kuwapokea Baadhi ya wak...

Wakati jamii nyingi zikihangaika kuhakikisha watoto wao wanapata elimu kwa namna yoyote ile, hali imekuwa tofauti kwa baadhi ya wazazi wengine ambao wamewakikataa watoto wao kuendelea na elimu ya juu kwa madai wao ni masikini

Picha
Wakati jamii nyingi zikihangaika kuhakikisha watoto wao wanapata elimu kwa namna yoyote ile, hali imekuwa tofauti kwa baadhi ya wazazi wengine ambao wamewakikataa watoto wao kuendelea na elimu ya juu kwa madai wao ni masikini Amos Mabula ambae ni mwalimu mkuu wa shule ya Nyakasanda , iliyoko Tarafa ya Mabamba wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma,  alipokuwa akiongea na clouds Tv, amesema kutokana na mwamko mdogo wa elimu, miongoni mwa baadhi ya wazazi, wamekuwa wakiwazuia watoto kufanya vizuri kwenye mihani yao kuhitimu elimu ya msingi kwa kisingizio kuwa wakifaulu wao hawana uwezo wa kuwasomesha Amesema kutokana na hali hiyo baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakichora picha za wanyama kwenye karatasi za kujibia mitihani japo majina yao uandikwa kwa usahii  Afisa elimu shule za msingi wilayani humo Joseph Tirutangwa, alipotembelea shule hiyo na kuongea  baadhi jamii amewataka kuachana na mawazo potofu kwani hali hiyo ni kuharibu maisha ya watoto wao Hata hi...