Mgombea wa urais wa Marekani kwa tikiti ya chama cha Republican Donald Trump ameimarisha kampeini zake mjini Nevada licha ya kisa cha usalama kilochobabisha walinzi wake kumuondoa jukwaani kwa muda.
Mgombea wa urais wa Marekani kwa tikiti ya chama cha Republican Donald Trump ameimarisha kampeini zake mjini Nevada licha ya kisa cha usalama kilochobabisha walinzi wake kumuondoa jukwaani kwa muda.
Wafuasi wake wanasema walinzi wake walifanikiwa kumuondoa jukwaani licha ya hofu kwamba kulikuwa na mtu aliyekuwa amejihami kwa silaha miongoni mwao.
Bw.Trump alikuwa anakaribia kilele cha hotuba yake ndani ya ukumbi wa Reno uliyojaa wafuasi wake, na ghafla kukatokea rabsha karibu na jukwaa.
Taharuki ilitanda mahala hapo kabla ya walinzi wake kufanikiwa kumuondoa.
Wafuasi wake waliyojawa na hofu walianza kukimbilia lango la kutoka nje wa ukumbi huo kufuatia madai ambayo hayakudhibitishwa
Polisi wamemkamata mtu mmoja kufuatia tukio hilo lakini akaachiliwa muda mfupi baadaye.
Mtu huyo hakupatikana na silaha kama ilivyodaiwa.
Huku zikiwa zimesalia siku tatu kabla ya uchaguzi mkuu,wagombea wote wawili wameimarisha kampeini zao katika jimbo muhimu la Florida linalo na umaarufu wa kuamua mshindi wa uchaguzi wa urais.
Kumekuwa na ongezeko la watu wa asili ya hispania wanaopiga kura mapema Florida na Nevada.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema huenda hatua hiyo ikamnufaisha Bi Clinton.
Trump amesema atazuru jimbo la Minnesota ambalo chama cha Republican hakijawahi kupata ushindi kwa zaidi ya miaka arobaini.
Maoni
Chapisha Maoni