Idadi ya wakimbizi raia wa Burundi wanaoendelea kuikimbia nchi yao kutokana na machafuko ya kisiasa yaliyoanza toka mwezi April mwaka jana nakupewa hifadhi katika kambi ya Nduta iliyopo wilayani Kibondo Mkoani Kigoma imeendelea kuongezeka siku hadi siku.
Idadi ya wakimbizi raia
wa Burundi wanaoendelea kuikimbia nchi yao kutokana na machafuko ya kisiasa yaliyoanza
toka mwezi April mwaka jana nakupewa hifadhi katika kambi ya Nduta iliyopo wilayani
Kibondo Mkoani Kigoma imeendelea kuongezeka siku hadi siku.
Hayo ya mebainishwa na mkuu
msaidizi wa kambi hiyo Bi Jeska Ntaita alipozungumza na Clouds fm kuhusiana na idadi ya wakimbizi wanaoendelea
kupokelewa kwenye kambi hiyo pamoja na changamoto kwenye kambi hiyo.
Amesema hadi sasa kambi
hiyo imepokea zaidi ya wakimbizi 55,500 (hamsini natano elfu na miatano) na kwamba
changamoto ya maji iliyokuwa ikiikabili kambi hiyo ikiwa inaendelea kushughulikiwa
Aidha Bi Ntaita amesema
kambi hiyo ilisimama kupokea wakimbizi hao kutokana na hapo awali kuwa natatizo
kubwa la uhaba wa maji na sasatatizo la hilo la limeshughulikiwa na sasa wana mpango
wakuendelea kuwapokea wakimbizi hao hadi kufikia 60,000 ilikupunguza msongamano
kwenye kambi zingine zinazoendelea kuwapokea
Baadhi ya wakimbizi wanaoendelea kupokelewa kwenye kambi
ya wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo Mkoani Kiggoma wamesema wanaendelea
kuimbia nchi yao kutokana na mauaji yanayoendelea kujitokeza katika nchi yao na
sio kwamba wanakimbia njaa kama inavyoelezwa na baadhi ya watu.
Maoni
Chapisha Maoni