Kibondo;Mkuu wa wilaya ya Kibondo mkoani kigoma Luis Bura amemwagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo kuwasimamisha kazi watumishi 3 wa idara ya ujenzi kutokana na ubadhilifu wa fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba ya walimu katika shule ya sekondari Itaba
Kibondo;Mkuu wa
wilaya ya Kibondo mkoani kigoma Luis Bura amemwagiza mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya wilaya hiyo kuwasimamisha kazi watumishi 3 wa idara ya ujenzi
kutokana na ubadhilifu wa fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba ya
walimu katika shule ya sekondari Itaba
Watumisha hao wanatuhumiwa kudanganya ili mkandarasi
anaejenga nyumba hizo kulipwa milion 109 malipo ya wamu ya pili kwa madai kuwa
ujenzi umekemilika kwa asilimi 85% ambapo milion 46 zimelipwa bila kufanyiwa
kazi yoyote huku ujenzi ukiwa chini ya viwango na ukiwa uko chini ya asilimia
50% kama alivyoeleza mkurugenzi wa halmashauri hiyo Juma Mlehe kwa waandishi wa
habari na wananchi
Mkuu huyo wa wilaya katika maelezo yake alisesema matatizo
ya ubadhilifu wa fedha za serikali katika wilaya hiyo yamekuwa ni mambo ya
kawaida huku akilalamikia makundi ya wanasiasa kuingilia shughuli za kitaalam
kwa kuwalazimisha watumishi wa halmashauri kufanya mambo wanayoyataka wao na kuwataka kufuata sheria na taratibu
Aidha Bura, alisema baada kupata malalamiko ya vitendo
vinavyofanywa na mkandara, waandisi walmashauri na baadhi ya wanasiasa, kamati
ya ulinzi na usalama ilifika katika eneo la ujenzi na kukuta kile kilichodaiwa
kuwa ujenzi umekamilika sivyo ilivyo kukuta vyoo ni mashimo madirisha hayapo
sakafu haijawekwa na kuamua mwaandisi
Salehe Mbogoye, Felix Ngomano na Haruni Mbapaye
‘’Madiwani hawa juzi waliomba posho ya kufanya ukaguzi wa
ujenzi huu wakapewa posho ya siku tano na hata kwenye ujenzi hawakufika hadi
leo jamani mambo hayo ni aibu, na kuongeza kuwa wengine wanaoangukiwa na mkasa
huo ni na kutakiwa kuandika barua za maelezo ni Afisa elimu sekondari Wilaya
Honolata Kabundugulu,Fedy Eliasafu afisa maliasili na Afisa kilimo wilaya Said
Shemahonge nazitaka barua hizo jumanne kwenye kikao alisema Bura’’
Hata hivyo viongozi wa vijiji mmoja wao Bosco Ngomagi
wameiomba serikali kuhakikisha wanashirikishwa mara miradi inapoingizwa katika
vijiji vyao ili ufuatiliaji na ushauri uweze kufanyika kwa ukaribu huku vibarua
na mafundi waliopewa kazi na kampuni iliyochukua kandarasi iliyofahamika kwa jina la Mangalazi
engnearing ya mjini kigoma wakiomba
msahada wa ufuatiliaji wa amalipo yao kwa kuwa fedha nyingi zimeshachukuliwa
alieleza Paschal Leonard
Ujenzi huo unagarimu
shilingi million 264 kwa ajili ya ujenzi
wa nyumba ya walimu yenye kuchukua familia sita Vyumba vitatu vya madarsa, vyoo
vitatu vya kisasa kwa ajili ya wanafunzi na walimu matundu mawili ambapo vyote
hivyo bado havija kamilika licha ya kudaiwa kuwatayari
Katika uchunguzi mdogo uliofanywa na Gazeti la Mwananchi
umebaini wapo baadhi ya madiwani ambao wamekuwa wakiwashawishi baadhi ya
watumishi wa halmashauri kuwapa fedha na
wanapokataliwa uanza kuwaandama kwa kuwaadhimia kwa madai watua hao hawafai na
kutaka wahame au wasimamishwe kazi hali
ambayo uenda ndiyo inayopelekea wengi wao kutofuata taratibu
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni