Wakati jamii nyingi zikihangaika kuhakikisha watoto wao wanapata elimu kwa namna yoyote ile, hali imekuwa tofauti kwa baadhi ya wazazi wengine ambao wamewakikataa watoto wao kuendelea na elimu ya juu kwa madai wao ni masikini
Wakati jamii nyingi zikihangaika kuhakikisha watoto wao
wanapata elimu kwa namna yoyote ile, hali imekuwa tofauti kwa baadhi ya wazazi
wengine ambao wamewakikataa watoto wao kuendelea na elimu ya juu kwa madai wao
ni masikini
Amos Mabula ambae ni mwalimu mkuu wa shule ya Nyakasanda ,
iliyoko Tarafa ya Mabamba wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma, alipokuwa akiongea na clouds Tv, amesema
kutokana na mwamko mdogo wa elimu, miongoni mwa baadhi ya wazazi, wamekuwa
wakiwazuia watoto kufanya vizuri kwenye mihani yao kuhitimu elimu ya msingi kwa
kisingizio kuwa wakifaulu wao hawana uwezo wa kuwasomesha
Amesema kutokana na hali hiyo baadhi ya wanafunzi wamekuwa
wakichora picha za wanyama kwenye karatasi za kujibia mitihani japo majina yao
uandikwa kwa usahii
Afisa elimu shule za msingi wilayani humo Joseph Tirutangwa,
alipotembelea shule hiyo na kuongea
baadhi jamii amewataka kuachana na mawazo potofu kwani hali hiyo ni
kuharibu maisha ya watoto wao
Hata hivyo mmoja wa wazazi Jacob Madaha, katika hatua ya kuelimishana, wakati mahafali
ya kuhitimu kidato cha nne katika shule ya sekondari Bon consilii iliyokoko
katika tarafa hiyo amewambia wazazi hao kuwa wanapaswa kwenda na mabadiliko ya
ulimwengu kwani mzigo wanao ukataa unaweza kuwaelemea zaidi hapo baadae pale
wasipowasomesha watoto wao
Nao baadhi ya wanafunzi wamekuwa na maoni mitazamo
mbalimbali wakiiomba serikali kulingana na mazingira zinakoishi baadhi ya jamii
ni bora zikawa zinatembelwa kaupewa elimu kwa ajili ya kunusulu vizazi vijavyo
huku wakiwataka wanafunzi kujitambua wao wenyewe
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni