Viongozi wa nchi za Afrika Magharibi wamempa Yahya Jammeh fursa ya mwisho kuachia madaraka, huku wanajeshi wa Senegal wakiingia nchini Gambia.
Habari za kuapishwa kwa Adama Barrow zilipokelewa kwa furaha na shangwe Banjul Adama Barrow baada ya kuapishwa aliwaamuru wanajeshi wa Gambia wasalie kambin Viongozi wa nchi za Afrika Magharibi wamempa Yahya Jammeh fursa ya mwisho kuachia madaraka, huku wanajeshi wa Senegal wakiingia nchini Gambia. Bw Jammeh amepewa hadi saa sita mchana Ijumaa kuachia madaraka la sivyo aondolewe kwa nguvu na wanajeshi wa nchi za Afrika Magharibi wanaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa. Wanajeshi hao wametakiwa kusubiri hadi makataa hayo yamalizike. Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (Ecowas) inaunga mkono Adama Barrow, ambaye aliapishwa kuwa rais mpya wa Gambia katika ubalozi wa nchini hiyo nchini Senegal. Jammeh aongezewa jina jingine Juhudi za mwisho za kumshawishi Bw Jammeh kuondoka kwa hiari, ambazo zinaongozwa na Rais wa Guinea Alpha Conde, zinatarajiwa kufanyika Ijumaa asubuhi. Mwenyekiti wa tume ya Ecowas, Marcel Alain de Souza, alisema iwapo mkutano huo u...