Kakonko;Madiwani wa wanaoongozwa na Chadema katika baraza la halmashauri ya Kakonko Mkoani Kigoma wamempa siku saba Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Juma Maganga kuandika barua ya kijieleza usahihi wa kupitisha rasimu ya Bajeti ya 2017/18 kinyume na taratibu na asipo fanya hivyo watamshitaki mahakamani
Add caption |
Dafroza Expelius mmoja wa madiwani Chadema |
Juma Maganga mwenyekiti Halmashauri ya Kakonko |
Medas Amos katibu kambi ya Chadema Halmashauri ya Wilaya Kakonko |
Kakonko;Madiwani
wa wanaoongozwa na Chadema katika baraza la halmashauri ya Kakonko Mkoani
Kigoma wamempa siku saba Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Juma Maganga kuandika
barua ya kijieleza usahihi wa kupitisha
rasimu ya Bajeti ya 2017/18 kinyume na taratibu na asipo fanya hivyo
watamshitaki mahakamani
Akiongea na Waandishi wa Habari jana Katibu wa Kambi wa
chadema wa madiwani Medas Amosi alisema kuwa mwenyekiti huyo alitumia mabavu
kupitisha rasimu hiyo kwa ikama isiyokamilika baada ya madiwani 8 wa chadema
kuikataa na kukubaliwa na madiwani 10 wa ccm kukubabali
‘’Kwa kutambua kuwa alienda kinyume na sheria, inayozipa
mamlaka na Madaraka serikali za mitaa kifungu cha183 sheria no7,na kifungu cha
97 sheria namba 8 ya mwaka 1982 tunataka mwenyekiti huyo atuleleze kwanini
aliamua kkukiuka taratibu na
tumemuandikia barua asipo jibu na
tusiporidhia tutakwenda mahakamani Amosi’’
Aidha Madiwani hao wa chadema waliongeza kuwa utaratibu
uliotakiwa kutumika ni Theruthi mbi ya wajumbe ambao ni 12 kwa mujibu wa sheria
badala yake waliopitisha rasimu hiyo ni 10 tu na kueleza sababu ya kuikata kuwa
ni kutokana na kuingiza kodi ya majengo kabla ya kupa maoni ya wananchi husika
Kwa upande wake Juma Maganga ambae ndiye anaelelemikiwa
amesema yeye alipitisha rasmu hiyo kwa ridhaa ya wajumbe walio wengi na
anashangaa wenzake wa chadema kuwa na malamamiko ya aina hiyo Bajeti kwa mujibu wa taratibu ilianzia ngazi
za chini kabisa kwa wananchi wakakubali, huku wana wengine wakiwataka viongozi
kuachana na marumbano ya siasa katika mambo ya maendeleo
‘’Madiwani wenyewe wanaolalamika ukiwauliza kwa nini
wanapinga rasimu hii wanadai inautaratibu kandamizi kwa kutoza kodi ya majengo
na ukiwauliza ni chanzo gani mbadala tuweke hawaelezi, na sasa watambue kuwa
swala la kodi ya majengo ni maamuzi ya serikali na bado yako kwenye rasimu nna
inatakiwa ipite katika ngazi zinazohusika alisema Maganga’’
Ikumbukwe kuwa tar 16.jan mwaka huu kilifanyika kikao cha
cha baraza la madiwani kwa ajili ya kujadili na kupitisha rasimu ya bajeti ambapo madiwani wa kambi ya upinzani
wanaoongozwa na chadema waliipinga kwa madai haija kidhi vigezo
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni