Kibondo;Idara ya elimu katika Halmashauriya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma inakabiliwa na tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa 138 kwa shule za msingi hali inayopelekea wanafunzi wengi kutembea umbali mrefu wakifuata elimu na kusababisha adha kwao na ufundishaji kuwa mgumu kwa walimu
Kibondo;Idara ya
elimu katika Halmashauriya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma inakabiliwa na
tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa 138 kwa shule za msingi hali
inayopelekea wanafunzi wengi kutembea umbali mrefu wakifuata elimu na kusababisha
adha kwao na ufundishaji kuwa mgumu kwa walimu
Vyumba hivyo vya madarasa vinavyohitajika, ni katika shule
24 za wilaya hiyo ambapo vinatarajia kugarimu kiasi cha Tsh bilion 1 na milion
300 huku shule zingine zikikosa vyumba kabisa na miundo mbinu yote kutokidhi
mahitaji.
Akitoa taarifa yake wa wakati wa uhamasishaji wa ujenzi wa
vyumba vya madarasa uliofanyika jana katika shule ya Msingi Nyamguruma
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo
Juma Mnwele alisema kutokana na hali
hiyo wameamua kuanzisha utaratibu wa kushirikiana wananchi katika shughuli za
ujenzi kawenye maeneo mbalimbali ya
wilaya hiyo ili kuwaboreshea walimu na wanfunzi mazingira ya jifunza na
kufundishia
Katika hafra hiyo ya uzinduzi wa ujenzi wa vyumba vya
madarasa mkuu wa wilaya hiyo Luis Bura ambae alikuwa mgeni rasmi alipokuwa
akizungumza na wananchi waliohudhulia alitoa wito kwa jamii na Viongozi kujenga Tabia ya kujitegemea katika shuguli
zao za maenedeleo ili serikali iweze kwaunga mkono katika hatua inayokuwa
ikiendelea
Walimu na wanafunzi ambao ni Zabron Kasato na Tmain Mayi walieleza
usumbufu wanaoupata kutokana na
kutembea umbali mrefu huku wakiupongeza uongozi wa halmashauri kwa
kuliona swala la uhaba wa miundo mbinu mashuleni hasa ukosefu vyumba vya madarasa na Nyumba za walimu wakiomba litiliwe mkazo ili kuonyesha
mafanikio
Aidha kutokana na serikali kutaka kuboresha elimu na kuondoa
malipo mwaka wanafunzi walioandikishwa kuanza darasa la kwanza katika wilaya ya
Kibondo 2017 ni asilimia 25 tofauti na mwaka jana kiwango kinachojwa kuwa cha
chini ambapo mkuu wa wilaya hiyo amewataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto shule na atakae kiuka atachukuliwa
hatua za kisheria
Licha ya maelezo ya
mkuu wa wilaya kuwachukulia hatua wazazi watakao kataa kuwandikisha watoto
wenye umri wa kwenda shule, Baadhi ya
Wazazi wamelalamikia Vitendo vya wanaume kukataa kutoa mahitaji kwa wanafunzi
na kukataa kuwaandikisha shule na kutelekeza familia zao walieleza Grace Joakim
na Ester Bahati
Hata hivyo imetajwa kuwepo na changamoto ya uelewa Mdogo kwa
baadhi ya wazazi juu maswala ya elimu kwa kukataa kuwapeleka watoto wao
mashuleni wapate elimu, na kushindwa kutoa mahitaji muhimu kwa kisingizio cha
uwezo mdogo na kuiomba serikali kuhamasisha jamii juu hilo
‘’ Wanaosomesha watoto kwamba ni watu wote wenye uwezo wa
kiuchumi bali ni uelewa wa wazazi na kuona umuhimu wa kusomesha watoto maana
tumeona watu wengine wakiuza mpaka mashamba yao kwa ajili ya kusomesha watoto
wao alisema Mwalimu Melina Kayogoma’’
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni