Kibondo;Baadhi ya Wakazi wa Mabamba wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma wameiomba serikali ya Tanzania kustisha utaratibu wa kupokea raia wa nchi ya Burundi wanaoingia hapa nchini kama wakimbiambi kwa kuwa hali ya utulivu na amani nchini mwao imesharejea
Luis Bura Mkuu wa wilaya ya Kibondo |
Everine Thadeo Twesa |
Thobias Sijabaje Ofisa mwakilishi wizara mambo ya Ndani Kitengo cha wakimbizi |
Kibondo;Baadhi ya Wakazi wa Mabamba wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma wameiomba serikali ya Tanzania kustisha utaratibu wa kupokea raia wa nchi ya Burundi wanaoingia hapa nchini kama wakimbiambi kwa kuwa hali ya utulivu na amani nchini mwao imesharejea
-
-
Wadai kuhofia makundi makubwa yanayiongia kwa
kasi kuwa ni chanzo cha vitendo vya
uharifu vinavyoenda ikiwemo uharifu wa mazingira kwa kukata miti hovyo kwa
ajili ya maandalizi ya makazi Makambini
-
-
Amos Degratias na Arcado Adam ambao ni wakazi
mabamba wakiongea na Gazeti hili jana katika Kijiji cha Nyakasanda kilichoko
mpakani mwa nchi ya Burundi na Tanzania
walisema kuwa hivi sasa katika nchiyo ya jirani amani iliyokuwa
imetoweka kutokana na vurugu za kiasasa imereje hivyo wimbi kubwa linaloendelea
kuingia hawana vigezo vya ukimbizi
-
-
‘’Kinachotutisha ni watu wengi badala ya kwenda
katika vituo vya kupokelea wakimbizi uishia vijijini na wanaoingia katika
Makambi ya wakimbizi baadae utoroka na kuanza kurudi nchini mwao bira taratibu
na wengi wanakimbia Njaa na hali ngumu ya maisha alisema Amos ‘’
-
-
Mwananchi liliweza kufika katika kituo cha Kupokelea
wakimbizi kilichoko katika kijiji cha Mkalazi
na kuona hali halisi ilivyo na kuongea
na baadhi ya wafanyakazi wa mashirika ya kuhudumia wakimbizi ambao aliulizwa
Ofisa mmoja wa shirika la Twesa, aliyejimbulisha kwa jina la Everin Thadeo na
kueleza kuwa idadi kubwa ya wakimbizi
wanaingia Tanzania katika siku za magulio jumamos na jumatano
-
-
Baadhi ya waomba hifadhi ambao ni Muwenayo Athumani Kimuga Said walipohojiwa
juu ya hali ilivyo nchini mwao na kinachowakimbiaza walisema wanavamiawa nyakati za usiku na
kupewa vitisho hali inayopelekea kuyakimbia makazi yao hali hali ngumu ya
Maisha
-
-
‘’ Tunapowauliza kwanini mnakuja siku za
jumatano na jumasi wanatueleza kuwa kwa siku za kawaida wanajeshi wa nchi yetu
utuzuia ila kwa siku hizo tunawambia kuwa tunenda masokoni kama kawaida kwa
mosoko ya ujirani mwema alisema Thadeo’’
-
-
Hata hivyo Afisa mwakilishi toka Wiazara ya Mambo
ya Ndani Kitengo cha wakimbizi Thobias Sijabaje alikiri kuwepo kwa idadi kubwa
ya wakimbizi wanaoingia nchini kuwa kuanzia mwezi desemba mwaka jana hadi sasa
wanapokea watu 463 kwa siku moja katika Vituo vya Mkalazi Lumasi na Mgunzu
-
-
Aidha Thobiasi aliongeza kuwa Tanzani ni moja ya
nchi zilizo saini mkata wa umoja wa Mataifa kuhusu waomba hifadhi nao wanapokea watu wanaosalimiasha roho zao
hivyo kutokana na mkataba huo hakuna mtu mwenye mamlaka ya kumrudisha mtu
anaekimbia kujisalimisha ila kwa sasa wataendelea kuwapokea huku taratibu za
kimataifa zikisubiliwa
-
-
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kibondo ambaye
pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo Luis Bura
alisema kuwa kinachosababisha watu wengi
kuingia Tanzani kama wakimbizi wakitoka nchini Burundi ni kwasabu walikia
shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa linatarajia kubadilisha
utaratibu wa kuwapa chakula badala yake litakuwa linatoa fedha kwa wakimbizi
wengi kuhadiwa kupewa hifadhi ulaya na Amerika
-
-
Bura aliongeza kuwa hivi sasa katika Kambi ya
wakimbizi ya Nduta iliyoko wilayani Kibondo inakaribia kujaa kwa kuwa na idadi
ya wakimbizi wapatao 90 elf na kusema kuwa italazimika kufungwa watakapofika
laki 120,000 kwa kuwa ndiyo uwezo wake baada ya hapo hakuna mkimbizi
atakayeruhusiwa kupelekwa kambini humo kwa kuhifadhiwa
-
-
Raia wengi wa nchi ya Burundi wamekuwa
wakiikimbia nchi hiyo kutokana na machafuko ya kisiasa baada ya Rais
Nkurunziza kutangaza kuwania muhula wa
tatu kugombea kiti hicho mwaka 20015
-
Mwisho
-
-
-
-
Maoni
Chapisha Maoni