Kakonko;Jamii imetakiwa kuacha tabia ya kuwabagua watoto wa kike kwa kupuuza kuwapeleka shule ili kupata haki yao ya msingi tofauti na watoto wa kiume wanavyopewa kipaumbele katika maswala ya Elimu ikidai kwa watoto wote nisawa na ni vema Mtoto wa kike akapwa umuhimuJoyce Ndalichako waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi alipotembelea wilayani Kakonko
Joyce Ndalichako waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi |
Joyce Mwakabibi mkurugenzi Halmashauri Kakonko |
a Maganga mwenyekiti Halmashauri KakonkoJum |
Kanal Hosea Ndagala Dc Kakonko |
Wananchi waliokuwa wakimsikiliza waziri wa elimu Joyce Ndalichako |
Kakonko;Jamii imetakiwa kuacha tabia ya kuwabagua watoto wa kike kwa kupuuza kuwapeleka shule ili kupata haki yao ya msingi tofauti na watoto wa kiume wanavyopewa kipaumbele katika maswala ya Elimu ikidai kwa watoto wote nisawa na ni vema Mtoto wa kike akapwa umuhimu
Mila na destili Mitazamo hasi na uelewa mdogo sababu zinazopelekea watu wengi kuwabagua watoto wa kike katika kuwapatia haki mbalimbali yakiwemo masomo
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi Joyce ndalichako jana wakati wa maadhimisho wa ya miaka 40 ya chama cha Mapinduzi yaliyofanyika katika Kijiji cha kasanda wilayani Kakonko Mkoa wa Kigoma ambapo alisema jamii imekuwa na mitazamo tofauti katika kumpatia elimu mtoto wa kike
‘’Nanyinyi watoto wa kike acheni kukimbilia mambo ya ya maisha kabla ya wakati wenu wa kuyafikia hayo mtayakuta mwanadamu ana muda mfupi sana kuwa shuleni kuliko maisha ya kawaida hivyo watoto tulien shikeni sana masomo ulimwengu bila elimu ni mgumu sana alisema Ndalichako’’
Aidha Ndalichako amewataka watanzania kuhakikisha wanadisha amani kwa kujitenga na migawanyiko isiyokuwa na tija kama ya kisiasa kidini na hata uvunjifu wa sheria za nchi akiwataka hasa wakazi wa mkoa wa kigoma kutazama mfano wa majira zao wanaoikimbia nchi yao kutokana na kuvunjika kwa amani
Kwa upande mwingine baadhi ya wananchi waliohudhulia mkutano huo ambao Philmon Salvatory na Ameli Paulo walielezea mitazamo ya baadhi yao kukataa kusomesha mtoto wa kike kuwa ni pamoja hali ambayo imekuwa ikikatisha tamaa baada ya msichana kugalimiwa fedha nyingi na baadae kushindwa kuendelea na masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo kubeba mimba akiwa shuleni ikiwa ni pamoja na uelewa mdogo
‘Licha ya mila na destuli hata hawa watoto wanakatisha Tamaa wazazi watu wengine tunafikia hatua ya kuuza mashamba ili mtoto asome matokeo yake unasikia alishatoroka shule na kwenda kuolewa hivyo hakuna anaewabagua wakati mwingine tunahuzunika sisi wazazi alisema Amelia’’
Pamoja na mambo mengine maadhimisho yaliambatana na kufanya shuguli za usafi katika mji wa kakonko ambapo waziri huyo alishiriki na wananchi wa wilaya hiyo kwa kufagia masokoni kufyeka nyasi katika maeneo ya kutolea huduma za afya
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni