Bujumbula; Baada ya hali ya amani kurejea nchini Burundi baada ya machafuko yaliyoyakumba baadhi ya maeneo hali iliyopelekea wananchi kuyakimbia makazi yao na utulivu kuweposasa, viongozi wa nchi hiyo wamewataka Raia walioko ukimbizin kurudi na kuendelea na maisha ya kawaida
Moja ya Mtaa katika mji wa Bujumbula Nchini Burundi |
wakazi wa Jiji la Bujumbula wakiendelea shuguli zao kama kawaida |
Abdalah Hasan ambae ni mkuu wa
Mkoa wa Ruyigi amesema hayo wakati kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya
Kibondo Mkoa wa Kigoma Tanzania ilipozulu nchini humo kwa ajili ya kudumisha
ujirani mwema kati ya Burundi na
Tanzania
Aidha liongeza kuwa baada ya
machafuko ya kisiasa ya mwaka 2015, hadi sasa watu bado wanakimbia kwa madai ya
kuwepo machafuko ambayo hivi sasa hayapo na kuwataka kurejea na kuipenda nchi
yao kwa kuwa Burundi itajengwa na kulindwa na warundi wenyewe
Nae Luis Bura ambae ni mkuu wa
wilaya ya Kibondo Tanzania, aliiomba
serikali ya Burundi kutengeneza mazingira ya kuwarudisha watu wake nchini mwao
kwakuwa amani imeshapatikana akidai wanaokimbia hawana sifa za ukimbiazi na
wameshazuia kupokea watu wasiyokuwa na sifa za ukimbizi kupokelewa katika kambi
zilizoko wilayani kwake
Katika Jiji la Bujumbula
linalodaiwa kukubwa sana na machafuko 2015 Gazeti hili lilishuhudia wakazi wake
wakiendelea na shuguli mbalimbali za kibiashara na nyinginezo bila wasi wasi na
kuzungumza na baadhi yao ambao ni Buchumi Shomali na Ngenda Banka ambapo walidai hivi sasa hakuna tatizo lolote wakiwataka ndugu zao kurudi nyumbani huku wakazi wa mkoa wa Ruyigi unaopakana na
Tanzania, Hamida Kharufan na Didas Luzovil wakisema kuwa inadaiwa wenzao
wanakimbia njaa tu warudi wafanyekazi wajenge nchi yao
‘’’Sisi hivi sasa nchi nzima ya
Burundi tunasafiri usiku kilometa nyingi bila kubugudhiwa na Mtu yeyote
kutokana na utulivu uliopo sasa hao wanaoendelea kuitoroka nchi yao wakimbia
nini warudi tujenge nchi yatu ukimbizi
si mzuri alisema Ngenda Banka’’
Kiongozi wa Jumhiya ya Vijana wa
Chama cha CNDD FDD, nchini humo Niyonashima Desire ambayo imekuwa ikituhumiwa
kuwasmbua raia wake na kudai wanawakimbia wao alipoulizwa kama tuhuma hizo ni za kweli amesema kuwa wao
siyo jeshi wala hawatishi watu ila wengi wao walikimbia kwa hofu na kushawishiwa na wanasiasa kwakuwa machafuko yalitolea zaidi Bujumbula
kwanini wa mikoa mingine waendelee kukimbia
Nchi ya Burundi iliingia katika
machafuko baada ya Rais wa nchi hiyo Piere Nkurunziza kutangaza kuwania muhula
wa Pili 2015 na kusababisha warundi wengi kukimbilia katika nchia za Uganga,
Rwanda na Tanzania
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni