Waumini wa Dini ya Kikristo na jamii kwa ujumla wametakiwa kufuata maadili ya mwenyezi Mungu kwa kuwa na upendo na kuwajali wengine ikiwa ni pamoja na familia na wote wasiyojiweza na kuondoa matabaka na kuhamsishana kufanya kazi
Waumini wa Dini ya Kikristo na jamii kwa ujumla wametakiwa kufuata maadili ya mwenyezi Mungu kwa kuwa na upendo na kuwajali wengine ikiwa ni pamoja na familia na wote wasiyojiweza na kuondoa matabaka na kuhamsishana kufanya kazi Wito huo umetolewa na Padre Simon Libeio ambaye ni Paroko wa Parokia ya Kalinzi Kigoma wakati wa Ibaada maalum iliyofanyika Parokia ya Mabamba Kimbondo kwa ajili ya Watawa wa Kike waliopata Daraja hilo ambapo amesema jamii nyingi hapa nchi zimepungukiwa upendo wa kumpenda Mungu na wanadamu ahli inayopelekea watu wengi kutojali familia na kuzama katika mambo ya utandawazi Simon ameongeza kuwa Wazazi wengi wameacha wajibu wao wa malezi kwa watoto hali inayopelekea kuwa na kizazi kisichokuwa na maadili hapo baadae huku baadhi ya waumini walioshiriki Ibada hiyo wakieleza kuwa kinachopelekea kuwepo hali hiyo ni ukosefu wa Imani na kutoka kufanya kazi ya kuongeza kipato cha familia na kupelekea umoja kutoweka H...