Mkutano wavunjika wananchi wakidai hadi Diwani wao aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha, wapewe maelezo yake alipo
Kibondo;Wananchi wa kijiji cha kagezi kata ya
kagezi wilayani kibondo mkoani kigoma wamegomea mkutano wa serikali ya kijiji kuendelea
baada ya kuibuka hoja wakitaka kujua diwani wa kata hiyo ambae pia ni mwenyekiti
wa halimashauri ya wilaya hiyo .Simoni Kanguye anayedaiwa kupotea katika
mazingira ya kutatanisha.
Diwani wa
Kata hiyo Simon Kanguye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya
Kibondo anadaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha tangu julai 20 mwaka
huu bado hapatikana licha ya juhudi kubwa za vyombo vya ulinzi kumtafuta
Wakizungumza
katika mkutano huo uliofanyika Kijijini
hapo jana baadhi ya wananchi ambao ni Stephan Ntabindi na Juma Bilampanye walisema
hawaoni haja ya kuendelea na ajenda nyingine na kujadili maendeleo ya kijiji chao
kwaku wa hawana kiongozi ambae atawafikishia kero,na hoja zao katika ngazi husika
hadi watakapopewa ufafanuzi.
‘’Hatuwezikujadili
maendeleo bila msimamizi maana hata kero zetu tukizitoa hapa hakuna mtu wa
kutuwasilishia na hakuna wa kusimamia miradi hiyo ya maenedeleo hivyo hatuko
tayari kuendelea na mkutano huu ahdi tupewe maelezo Diwani wetu kama aliungwa
au alifariki dunia’’ alisema Juma
Licha ya
mtendaji wa kijiji hicho Shaban Mohamed kuwataka wananchi hao kutulia ili wajadili maendeleo ya kijiji chao.
walikataa mkutano huo kuendelea ambapo walimtaka mtendaji wa kata Apolinaly
Stephen kutoa maelezo
Hata hivyo mtendaji huyo wa kata alisema yeye hana
maelezo yoyote kwa sababu nafasi yake ni
ndogo juu ya hilo huku mwenyekiti wa kijiji Zabron Ntimba akisema kuwa swala
hilo mwenye uwezo wa kulisemea ni mkuu a wilaya ambaye ni mwenyekiti wa kamati
ya ulinzi na usalama ya wilaya kuwataka kuendelea hatua iliyosababisha
mzozo mkali
Pamoja na
kupewa maelezo kuwa wanatakiwa wajadili namna ya kushiriki ujenzi wa zahanati
ya kijiji kwakuwa wamepata mfadhili wasije wakapokonywa msahada huo walikataa
katakata hali iliyopelekea mwenyekiti kufunga mkutano baada ya mzozo kuwa
mkubwa
Mmoja wa wananchi walokuwa wakilalamikia upotevu wa Diwani wa Kata ya Kagezi |
Shaban Mohamed mtendaji wa Kijiji Kagezi |
Zabron Ntimba mwenyekiti Kijiji Kagezi |
‘’Hilo jambo
ni kubwa sisi ngazi ya kijiji hatuwezi kulitolea maelezo naomba tuliache
tuendelee na agenda zetu maana hilo si moja ya ajenda zetu mmeliingiza bila
utaratibu na kwakuwa mmekataa tusiendelee, basi msimlaumu mtu pale kazi
zitakapokuwa zimekwama alisistiza Ntimba mwenyekiti wa Kijiji’’
Mkuu wa polisi mkoa wa kigoma redinad Mtui
hivi karibu alipokuwa akiongea waandishi wa habari juu ya kupotea kwa
mwenyekiti huyo. Alisema kuwa haiahamiki alipotelea wapi ila baada ya oisi yake
kupata taarifa za kupotea kwake wajitahidi sana kumtafuta bado hajapatika japo
bado jitiada zinaendelea kuhakikisha anapatikana
Maoni
Chapisha Maoni