Waumini wa Dini ya Kikristo na jamii kwa ujumla wametakiwa kufuata maadili ya mwenyezi Mungu kwa kuwa na upendo na kuwajali wengine ikiwa ni pamoja na familia na wote wasiyojiweza na kuondoa matabaka na kuhamsishana kufanya kazi
Waumini wa Dini ya Kikristo na jamii kwa ujumla wametakiwa
kufuata maadili ya mwenyezi Mungu kwa
kuwa na upendo na kuwajali wengine ikiwa ni pamoja na familia na wote
wasiyojiweza na kuondoa matabaka na kuhamsishana kufanya kazi
Wito huo umetolewa na Padre Simon Libeio ambaye ni Paroko wa
Parokia ya Kalinzi Kigoma wakati wa Ibaada maalum iliyofanyika Parokia ya
Mabamba Kimbondo kwa ajili ya Watawa wa
Kike waliopata Daraja hilo ambapo amesema jamii nyingi hapa nchi zimepungukiwa
upendo wa kumpenda Mungu na wanadamu ahli inayopelekea watu wengi kutojali
familia na kuzama katika mambo ya utandawazi
Simon ameongeza kuwa Wazazi wengi wameacha wajibu wao wa
malezi kwa watoto hali inayopelekea kuwa
na kizazi kisichokuwa na maadili hapo baadae huku baadhi ya waumini
walioshiriki Ibada hiyo wakieleza kuwa kinachopelekea kuwepo hali hiyo ni
ukosefu wa Imani na kutoka kufanya kazi ya kuongeza kipato cha familia na
kupelekea umoja kutoweka
Hata hivyo swala la
mmomonyoko wa maadili umekuwa ukisukiwa kwa vijana na baadhi ya wazazi ambapo
baadhi ya vijana wilayani Kibondo wamesema tatizo hilo liko vijana licha ya
baadhi ya wazazi kutoa maelekezo ya makuzi na huku wengine wakiwalaumu baadhi
ya wazazi kuwabagua watoto wa kike
Maoni
Chapisha Maoni