Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2018
Picha
Kijana aliyemea mkia afanyiwa upasuaji India Kijana mwenye mkia wa sentimita 20 unaomea chini ya uti wa mgongo wake amefanyiwa upasuaji ili uondolewe Ulianza kutokea katika mgongo wa kijana huyo wa miaka 18 baada ya siku yake ya kuzaliwa ya 14. Yeye na familia yake kutoka Nagpur nchini India walifanya swala hilo kua siri kwa sababu walikuwa na wasiwasi angechokozwa na wenzake. Sasa wanataka kuonana na daktari baada ya mkia huo kuendelea kumea mfupa ndani yake. Mkia huo unadaiwa kuwa mrefu kuwahi kutokea kwa mwanadamu ijapokuwa visa kama hivyo ni vichache. ''Ulianza kuwa tatizo baada ya kuanza kumea nje ya mwili wake'',alisema mamake ambaye hakutaka kutajwa jina. ''Angeinua mkia huo kila mara alipotaka kubadilisha nguo zake.Ningeona kwamba ilikuwa inakera na uchungu mkubwa kwake,kwa hivyo nilimpeleka hospitali''. Madaktari wanasema kuwa kijana huyo huenda alimea mkia huo ndani ya tumbo la mamake kutokana na kasoro ya uti wa mgongo,lakini

Mwili wa Akwelina waagwa

Picha
Mwili wa mwanafunzi aliyepigwa risasi juma lililopita Akwelina Akwilini umeagwa na kusafirishwa kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi siku ya Ijumaa wiki hii. Katika ibada ya heshima za mwisho ilyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha usafirishaji Tanzania NIT hapo Padri Raymond Mayanga wa Parokia ya Yohane Mbatizaji Luhanga, amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kumsaka mtu aliyempiga risasi mwanafunzi huyo Akwelina Akwilini, na kumuweka wazi ili awaombe radhi Watanzania. Akwelina Akwilini alipigwa risasi na Polisi juma lilopita siku ya Ijumaaa wakati kikosi cha polisi kitengo cha kutiliza ghasia,FFU, kilipokuwa kikiwakabili waaandamanaji wa chama cha upinzani cha CHADEMA baada ya kumaliza Kwa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Kinondoni,jijini Dar es salaam. Katika ibada hiyo pia liliibuka kundi la wanafunzi wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali wakitaka haki itendeke, mabango ambayo waliyainua p Mamia ya Watanzania wajitokeza kwenye viwanja vya Chuo

Mwanamume atolewa uvimbe wa kilo 1.8 kwenye ubongo India

Picha
Madaktari nchini India wamefanya upasuaji wa kipekee na kuondoa uvumbe wa uzani wa kilo 1.8 kutoka kwa mwanamume wa umri wa miaka 31. Wanasema huo huenda ukawa uvimbe mkubwa zaidi kuwahi kutolewa kwenye ubongo wa binadamu. Upasuaji huo, ambao ulidumu saa saba, ulifanyika mnamo 14 Februari katika hospitali ya Nair mjini Mumbai magharibi mwa nchi hiyo. Lakini taarifa za upasuaji huo hazikutangazwa moja kwa moja kwa sababu madaktari  "Sasa ni suala tu lake kupona, lakini maisha yake hayamo hatarini tena," Dkt Trimurti Nadkarni, mkuu wa upasuaji wa mfumo wa neva, ameambia BBC. Santlal Pal, mwuzaji duka kutoka jimbo la Uttar Pradesh kaskazini mwa India, amekuwa akiishi na uvimbe huo kwa miaka mitatu. Madaktari wanasema Pal alipoteza uwezo wake wa kuona kutokana na uvimbe huo. Hata hivyo, kuna matumaini kwamba huenda akapata uwezo wa kuona tena baada ya kupona.  na uhakika iwapo ulifanikiwa. Mke wake ameambia gazeti moja India kwamba alikuwa ameambiwa na madaktari ka

Kasulu;Idadi ya Vifo vinavyotokana na ugonjwa Malaria vimekuwa vikiongezeka katika hospitali ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma, kutokana na sababu mbalimbali ususa kwa Watoto chini ya umri wa miaka mitano ikilinganishwa na magonjwa mengine

Picha
Kasulu ;Idadi ya Vifo vinavyotokana na ugonjwa Malaria vimekuwa vikiongezeka katika hospitali ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma, kutokana na sababu mbalimbali ususa kwa Watoto chini ya umri wa miaka mitano ikilinganishwa na magonjwa mengine Vifo vinadaiwa kuongezeka kwa aslimia 48 hali iinayodaiwa kuwa ni hatari sana kwa maisha ya watu kutoka na ugonjwa huo wa malaria  Mganga mkuu wa Halmashauri ya mji  ya Mji wa Kasulu Mshana Dastan alisema hayo jana katika kikao cha baraza la Madiwani kilichoketi kujadili bajeti ya mji huo ongezeko hilo linaonekana kuwa kubwa kutokana na hospitali hiyo kuhudumia halmashauri zaidi ya nne mkoani kigoma zisizokuwa na hospitali ambazo Ni Buhigwe, Uvinza, Kaulu Vijijini, Kigoma vijijini na baadhi ya maeneo ya wilaya kibondo   Aidha Mshana alisema  kuanzia  mwezi julai hadi desemba 2017 vilitokea vifo 44 watoto chini ya miaka 5 na vifo 16   vilitokana na ugonjwa wa malaria  huku watu wazima julai hadi desemba vikiwa ni vifo 19 na 6 ni malaria

Watumishi wa idara ya mahakama wametakiwa kufanya kazi zao kwa weledi kama taratibu na sheria zinavyoelekeza ili kuondoa malalamiko wak wananchi na kuleta ufanisi kwa chombo hicho kinachotegemewa kwa utoaji wa haki hapa nchini

Picha
  Hosea NdagalaKaimu Mkuu wa wilaya Kibondo aliyesimaa aliyekuwa mgeni rasmi katika sherhr hiyo   Watumishi wa idara ya mahakama wametakiwa kufanya kazi zao kwa weledi kama taratibu na sheria zinavyoelekeza ili kuondoa malalamiko wak wananchi na kuleta ufanisi kwa chombo hicho kinachotegemewa kwa utoaji wa haki hapa nchini Kaulihiyo ilitolewa jana na kaimu mkuu wa wilaya  kibondo Hosea Ndagala wakati wakilele cha maadhimishoya wiki ya sheria ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo feb 1 kwa kutoa elimu mbalimbali juu ya sheria kwa wananchi  ambapo amesema changamoto zilizopo ni vema  zikawa fulsa kwa kujenga uelewa kuondoa usumbufu kwa wananchi na kuwalimisha juu ya matumizi ya teama Ndagala alisema utendaji usiofuata weledi hasa katika maswala ya utoaji haki kwa jamii ni moja ya sababu zinachangia kurudisha nyumba maendeleo kwani watu wengi ushindwa kufanya kazi zao kwa utulivu ikiwemo uchekeweshwaji wa kesi hivyo mwaka huu mpya wautumie vema kaatika kut