Kasulu;Idadi ya Vifo vinavyotokana na ugonjwa Malaria vimekuwa vikiongezeka katika hospitali ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma, kutokana na sababu mbalimbali ususa kwa Watoto chini ya umri wa miaka mitano ikilinganishwa na magonjwa mengine
Kasulu;Idadi ya Vifo vinavyotokana na ugonjwa Malaria vimekuwa vikiongezeka katika hospitali ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma, kutokana na sababu mbalimbali ususa kwa Watoto chini ya umri wa miaka mitano ikilinganishwa na magonjwa mengine
Vifo vinadaiwa kuongezeka kwa aslimia 48 hali iinayodaiwa kuwa ni hatari sana kwa maisha ya watu kutoka na ugonjwa huo wa malaria
Mganga mkuu wa Halmashauri ya mji ya Mji wa Kasulu Mshana Dastan alisema hayo jana katika kikao cha baraza la Madiwani kilichoketi kujadili bajeti ya mji huo ongezeko hilo linaonekana kuwa kubwa kutokana na hospitali hiyo kuhudumia halmashauri zaidi ya nne mkoani kigoma zisizokuwa na hospitali ambazo Ni Buhigwe, Uvinza, Kaulu Vijijini, Kigoma vijijini na baadhi ya maeneo ya wilaya kibondo
Aidha Mshana alisema kuanzia mwezi julai hadi desemba 2017 vilitokea vifo 44 watoto chini ya miaka 5 na vifo 16 vilitokana na ugonjwa wa malaria huku watu wazima julai hadi desemba vikiwa ni vifo 19 na 6 ni malaria na sabau ni kuchelewa kufika hospitali licha ya kuwepo kwa dawa na vitengani kwa ajili ya ugonjwa huo
Wakiongea kaitkakikao hicho,diwani kata ya Muganza Ezron Budulege alihoji mikakati ya idara ya afya kudhibiti hali hiyo kwa sasa ni ipi ili kunusulu maisha ya watu
''Mikakati tuliyonayo ni kutoa elimu juu ya wazazi na wananchi wote kuwahi hospitali mara mtoto au mtu mzima anapokuwa na tatizo, kunyunyizia dawa ya kuuwa vimelea vya malaria kwenye madimbwi na mabwawa na kutumia kwa usahihi vyandarua wanavyopewa'' alisema Ms
hana
Evance Bichunko Diwani Kata ya Msambala |
Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu wakiwa kwenye kikao cha Baraza kujadili Bajeti 2018/19 |
Dr Mshana Dastani mganga mkuu wa mji wa Kasulu |
fatina Husein Murugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu |
Daniel Nsanzugwanko Mbunge wa Kasulu Mjini |
hana
Wagonjwa wanaodaiwa walioripoti hospitalini hapo watoto chini ya miaka mitano ni 17801 octoba hadi desemb na watu wazima ni 19507 waliokutwa na ugonjwa huo, huku vipaumbele vya bajeti hiyo ya shilingi Bilion 38 vikiwa ni Afya Elimu na Maji walieleza Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji Fatina Husein na Mbunge jimbo la Kasulu Kasulu mjini Daniel Nsanzugwanko
''Kwakweli bajeti haiwezi kumaliza kila kitu ila kwa jitihada na mpagilio mzuri tunaweza kufikia malengo tutahakikisha tunashirikiana na wananchi wa jimbo hili katika ujenzi wa miradi ya maendeleo ili kupunguza changamoto zilizopo hasa upande wa afya elimu na tunataraji ifikapo feb15 mwaka huu wanafunzi waliokuwa wamebaki kwa kukosa vyumba vya madarasa watakuwa wameanza masomo kidato cha kwanza'' alisema Nsanzugwanko maana hivi sasa tumesha pata vyumba 18
Bajeti ni Mchakato ambapo uanzia ngazi ya chini kwa wananchi watu wengi wakikaa na kujadili kulingana na mahitaji ya maeneo husika lakini hapa hivi sasa baadhi ya madiwa ni walipokea kwa mawazo tofauti wakidai ni kulingana shida zinazowakabili wananchi hasa kwa upande wa afya na majialieleza Evance Bichonko Diwani Kata ya Msambala
Kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 1021 inaonekana mji wa Kasulu kuwa na Idadi ya watu 236,751 japo inadaiwa kuwepo na ongezeko la Watu kwa asilimia 4% kilamwa
Maoni
Chapisha Maoni