Mwili wa Akwelina waagwa

Mwili wa mwanafunzi aliyepigwa risasi juma lililopita Akwelina Akwilini umeagwa na kusafirishwa kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi siku ya Ijumaa wiki hii.
Katika ibada ya heshima za mwisho ilyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha usafirishaji Tanzania NIT hapo Padri Raymond Mayanga wa Parokia ya Yohane Mbatizaji Luhanga, amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kumsaka mtu aliyempiga risasi mwanafunzi huyo Akwelina Akwilini, na kumuweka wazi ili awaombe radhi Watanzania.
Akwelina Akwilini alipigwa risasi na Polisi juma lilopita siku ya Ijumaaa wakati kikosi cha polisi kitengo cha kutiliza ghasia,FFU, kilipokuwa kikiwakabili waaandamanaji wa chama cha upinzani cha CHADEMA baada ya kumaliza Kwa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Kinondoni,jijini Dar es salaam.

Katika ibada hiyo pia liliibuka kundi la wanafunzi wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali wakitaka haki itendeke, mabango ambayo waliyainua p

Mamia ya Watanzania wajitokeza kwenye viwanja vya Chuo cha usafirishaji Tanzania NIT kuaga mwili wa mwanafunzi

unde Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako alipo anza kuzungumza. Lakini pingamizi lao likasitishwa na askari awalio chukua mabango hayo na kuyachana.
Maadhimisho Haya ya ibada misa takatifu yamehudgiriwa na viongozi mbali mbali wa chama na serikali wakimwo Waziri wa Elimu Prof Joyce Ndaluchako na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Enjinia Hamad Masauni.

Chanzo ni bbc

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao