Mwanamume atolewa uvimbe wa kilo 1.8 kwenye ubongo India

Madaktari nchini India wamefanya upasuaji wa kipekee na kuondoa uvumbe wa uzani wa kilo 1.8 kutoka kwa mwanamume wa umri wa miaka 31.
Wanasema huo huenda ukawa uvimbe mkubwa zaidi kuwahi kutolewa kwenye ubongo wa binadamu.
Upasuaji huo, ambao ulidumu saa saba, ulifanyika mnamo 14 Februari katika hospitali ya Nair mjini Mumbai magharibi mwa nchi hiyo.
Lakini taarifa za upasuaji huo hazikutangazwa moja kwa moja kwa sababu madaktari "Sasa ni suala tu lake kupona, lakini maisha yake hayamo hatarini tena," Dkt Trimurti Nadkarni, mkuu wa upasuaji wa mfumo wa neva, ameambia BBC.
Santlal Pal, mwuzaji duka kutoka jimbo la Uttar Pradesh kaskazini mwa India, amekuwa akiishi na uvimbe huo kwa miaka mitatu.
Madaktari wanasema Pal alipoteza uwezo wake wa kuona kutokana na uvimbe huo.
Hata hivyo, kuna matumaini kwamba huenda akapata uwezo wa kuona tena baada ya kupona. na uhakika iwapo ulifanikiwa.
Mke wake ameambia gazeti moja India kwamba alikuwa ameambiwa na madaktari katika hospitali tatu tofauti Uttar Pradesh kwamba uvimbe huo hauwezo kuondolewa.
"Visa kama hivyo huwa hatari sana," Dkt Nadkarni alisema, na kuongeza kwamba Pal alihitaji painti 11 za damu wakati wa upasuaji huo.
Aidha, alitumia mtambo wa kumsaidia kupumua kwa siku kadha baada ya upasuaji huo.Chanzo cha habarii ini Bbc
Pal alipofuka kutokana na uvimbe huo

Pal na mkewe baada ya upasuaji

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji