Watumishi wa idara ya mahakama wametakiwa kufanya kazi zao kwa weledi kama taratibu na sheria zinavyoelekeza ili kuondoa malalamiko wak wananchi na kuleta ufanisi kwa chombo hicho kinachotegemewa kwa utoaji wa haki hapa nchini
Hosea NdagalaKaimu Mkuu wa wilaya Kibondo aliyesimaa aliyekuwa mgeni rasmi katika sherhr hiyo |
Kaulihiyo ilitolewa jana na kaimu mkuu wa wilaya kibondo Hosea Ndagala wakati wakilele cha maadhimishoya wiki ya sheria ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo feb 1 kwa kutoa elimu mbalimbali juu ya sheria kwa wananchi ambapo amesema changamoto zilizopo ni vema zikawa fulsa kwa kujenga uelewa kuondoa usumbufu kwa wananchi na kuwalimisha juu ya matumizi ya teama
Ndagala alisema utendaji usiofuata weledi hasa katika maswala ya utoaji haki kwa jamii ni moja ya sababu zinachangia kurudisha nyumba maendeleo kwani watu wengi ushindwa kufanya kazi zao kwa utulivu ikiwemo uchekeweshwaji wa kesi hivyo mwaka huu mpya wautumie vema kaatika kutenda haki
Akisoma lisara mahakamani hapo hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya hiyo Erick Marey amesema katika mwaka huu wiki ya sheria wameweza kutoa elimu kwa wananchi 6000
Amesema licha ya matarajio ya mafanikio ya Mfumo wa Tehama zipo changamoto ambazo zinaweza kuvujisha siri za mahakama kama kesi kuwa wazi kabla ya wakati mambo mengi ya mahakama ni ya siri lakini yamejipanga kukabiliana na tatizo hilo
Nae mwakilishi wa chama cha wanasheria wilayani kibondo Godrian Tilya amesema yapo makundi manne ambayo ukwamisha ufanisi wa mahakama na kusababisha usumbufu kwa wananchi akisema ni vema yakajirekebisha ambapo ametataja kuwa ni Polisi, mawakiri wa serikali na wa kujitegemea na mahakama yenyewe
‘’Sisi baadhi ya mawakili hasa wa kujitegemea tumekuwa na ujuaji mwingi katika kutete wananchi na kuwa na kesi zaidi ya mbili katika mhakama tofauti hali inayopelekea kuchelewa kwa mashauri mahakamani na polisi uchelewa kuleta mahabusu mahakamani kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mafuta ya magari ila ni vizuri tukabadirika ndipo utaratibu huu wa Tehama utaleta tija kiutendaji’’ alisema Tilya
Kwa upande wao baadhi ya wananchi ambao ni Meshack Ruhenda na Mapindizi Yusuphu waliudhuria sherehe hizo waiiomba serikali kupitia mahakama kupeleka elimu vijijini juu ya kutambua haki ya mwananchi katika kutoa ushahidi kwa kesi mbalimbali Insert Mapinduzi Yusuph na
‘’Wananchi uogopa kufika mahakamani kutoa ushahidi wakihofu kuwa uenda mambo yakawabadirikia mwishowe wakajikuta wanausumbiliwa na kufungwa hata kama wnafahamu mambo wanayotakiwa kuyatolea ushahidi mwisho wake kesi kuchelewa au kuiingizia serikali hasara zisizokuwa na sababu’’ alisema Ruhenda
Maoni
Chapisha Maoni