NMB kupunguza changamoto Madawati Shule za Msingi Wilayani KibondoFrolence Samizi Mbunge wa Muhambwe akisa
Frolence Samizi Mbunge wa Muhambwe alipokuwa akiongea na wakazi wa Busunzu |
Seka Urio Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi Tabora alipokuwa akitoa salam zake wakati wa hafla ya makabidhiano shule ya Msingi Busunzu B |
Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Kanali Agrey Magwaza |
Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Aggrey Magwaza akikabidhiana Madawati ya shule ya Msingi yaliyotolewa Na Benki ya NMB kulia ni Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Magharibi Seka Urio |
Kibondo. Shule ya Msingi Busunzu B iliyoko
Wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma yenye Idadi ya Wanafunzi 2980, inakabiliwa na
Changamoto Mbalimbali ikiwa ni pamoja na uhaba wa Madawati hali ambayo imekuwa
ikisababisha usumbufu kwa wanafunzi wakati wa ujifunzaji
Shule hiyo
ina Madwati 565 na inaupungufu wa Madawati 421 huku uhitaji ni Madawati 985 ambapo
wanafunzi wa shule hiyo wameeleza changamoto hiyo ambavyo imekuwa
ikiwasbabishia adha kubwa
Wanafunzi wa shule hiyo Jaclin Jeremia na Kefa Buzingu katika wamesema Dawati moja
wamekuwa wakikaa Watu 5 badala ya Watatu huku wengine wakikaa chini na wengine kukalia Mawe na Matofali
‘’Tunapata
adha kubwa sana wakati wa kujifunza mfano kama sisi kama sisi Wasichana Nguo zetu zimekuwa zikichafuka
sana na kutufanya tujisikie vibaya na miandiko yetu uharika ila alisema Jcklin Mwanafunzi
B
Katika kukabiliana na hali hiyo Benki ya NMB
imetoa Madawati 50 yenye thamani ya shilingi million tano ambapo Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Magharibi hiyo Seka Urio amesema wanafanya hivyo ili
kuunga Mkono serikali juhudi zake za kuboresha elimu
Aidha Seka
ameongeza kuwa wamekuwa wakitoa gawio la faida inayopatikana na kuirudisha
katika jamii ili kusaidia Nyanja mbalimbali katika utoaji huduma kwa Wananchi
ambapo ameeleza kuwa kwa mwaka huu Benki hiyo imeshato sehemu ya faida asilimia
1% ambayo ni sawa na Sh 6 Bilion nchi nzima
Kwa upande
wake Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Frolence Samizi amepongeza Mahusiano mazuri
yaliyopo kati ya Viongozi wa Serikali na Benki hiyo ambayo yamelekea kupatikana
kwa Madawati hayo ambayo yatapunguza changamoto iliyokuwepo shuleni hapo
Hata hivyo
Mbunge huyo aliwataka wanafunzi kutambua Jitada kubwa zinazofanywa na serikali
kwa kushirikiana na Wadau akiwataka kusoma kwa bidii huku akiwataka Wadau
wengine kama Mashirika na Benki zingine na kutoa michango yao kuboresha
miundombinu ya Elimu na Sekta zingine hapa nchini
Akipoke Madawati
hayo kutoka Benki ya NMB Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Kanali Aggrey Magwaza
amewataka wanafunzi kupenda elimu ili jitiada za serikali na Wadau za kuboresha
miundombinu ziweze kuleta tija kwani Elimu ndiyo msingi pekee wa kumkwamua
Binadamu katika lindi la umasikini huku akitoa wito kutunza vifaa vinavyotolewa
na Wadau ikiwemo serikali ili viweze kutumika kwa muda mrefu
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni