Wahitim Jkt wahaswa kuchangamkia Fursa zinazoibuliwa na serikaliVijana Jkt Mtabila Kikosi 825
Wahitim Jkt Kikosi 825 Mtabila wakiwa kwenye Paredi siku ya kufunga mafunzo |
Patrick Ndwenya Mkuu wa Kikosi 825 Mtabila |
Isack Mwakisu Mkuu wa Wilaya ya Kasulu alipokuwa akiwahubia mamia ya wananchi wakati wa kufunga Mafunzo ya awali ya Kijeshi mujibu wa sheria Mtabila 825 |
Kasulu.Vijana Nchini wametakiwa kuchangamkia
Fursa zinazotolewa na serikali kama Kilimo na Ujasiriamali, ili kukabiliana na
changamoto za ajira waweze kujikimu kimaisha
Akiwa
kwenye Hafla ya Kufunga mafunzo ya awali ya Kijeshi Vijana mujibu wa
sheria Oparasheni Miaka 60 ya Jkt Kikosi 825 Mtabila, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu
Mkoani Kigoma Isack Mwakisu amesema Vijana waache kutegemea kazi za maofini
bali wafanye kazi mbalimbali kulingana na ujuzi wao
Aidha aliongeza kuwa lipo pia tatizo la
upatikanaji wa mitaji lakini wakifuata miongozo na taratibu nzuri wanaweza
kupata mikopo kutoka Taasisi mbalimbali za fedha ikiwa ni pamoja na mikopo
inayotolewa katika Halmashauri na Majiji hapa nchini
‘’Nawambia nyinyi vijana mkiweza kujitambua na
mkawa na bidii kujituma katika shughuli zenu za Mikono mtafanikiwa na nyie
mtakaoendelea katika Vyuo mbalimbali mnatakiwa kusoma kwa bidii huku
mkitanguliza uzalendo katika nchi yenu’’alisema Mwakisu
Nae Mkuu wa Kikosi 825 Kj Mtabila Patrick Ndwenya amesema Vijana
waliopokelewa Kikosini hapo wamejifunza mambo mbalimbali kama Kilimo na ufugaji
Nyuki na kuwataka kutumia ujuzi huo na
kuelemisha Vijana wenzao maali popote watakapokuwa
Aliongeza kuwa
Vijana hao katika kipindi cha miezi mitatu walipokuwa kikosini hapo
waliaandaa shamba la Mahindi lenye ukubwa wa Hekali 400 na Mizinga ya nyuki 400
baada ya kujifunza masuala ya ufugaji nyuki
Baadhi ya Vijana waliohitimu Kikosini ahapo ambao
ni Emmanuel Marwa na Restuta
Mwakifuna wamepongeza hatua hiyo ya mafunzo kwani imewajengea uwezo wa kufanya
mambo ambayo walikuwa hawayawezi kama kulima na hata kuchangamana na wenzao kwa
kushirikiana kulingana na mazingira ya maisha ya familia walikotoka, huku
wakiahidi kuwa waadilifu popote watakapokuwa
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni