Wanawake Jitambueni kufanya kazi
Wanawake Jitambueni kufanya kwa kujituma kazi
Kibondo.Wanawake wamehaswa kujituma katika kufanya kazi ili kuogeza vipato vya familia na kuboresha malezi ya watoto ili kuepukana na ukatili wa kiuchumi na kijinsia
Wengi wao wametajwa kutumia mitandao na kuiga tamaduni zisizostaili hatua ambayo imekuwa ikiwachelewesha kufikia malengo yao na kusababisha kukata tamaa
Wakiwa katika siku 16 za kupinga ukatili, kwenye hafla iliyo wahusisha Wanawake wanachama wa Kibondo women Gala cha Mkoani Kigoma Mwalimu wa Masuala ya Kisaikolojia Epsalia Malya amesema wanawake wengi wamekuwa wavivu wa kujishuguli huku wakipendelea kujipamba na kushindwa kufanya kazi
‘’Aliyeajiriwa afanye kazi kwa weredi kwa kufuata taratibu za kazi Mfanyabiashara nae awe mbunifu kwani umakini na kujali ni moja chanzo cha mafanikio kwa mlengwa na hizo ndizo baraka’’alisema Malya
Nae Sadaka Gandi toka Jijini Dsalaam ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ambae pia ni Mtaalam wa Saikolojia amesema zipochangamoto nyingi zinazikabili jamii hasa wanawake kutokana na kutojitambua ambapo amewataka wanandoa wote kuheshimiana na kuwataka wanaume kutokaa kimya pale wanafanyiwa ukatili
Chama hicho cha wanawake Kibondo kilianzishwamwaka 2023 kwa lengo la kutoa elimu kwa kuyashirikisha makundi ya wajasiriamali, watumishi wa serikali na mashirika ili kufanya shuguli zao kitaalam badala ya mazoea hali ambayo imekuwa ikisababisha wengi wao kutofanikiwa ipasavyo
Mwenyekiti wa Chama hicho Doreen Lyimo amesema tangu kuanzishwa kwake na kuwapa elimu wanawake namna ya kufanya kazi kulingana na mazingira yao ya kazi ikiwa ni pamoja na malezi ya familia na wengi wamenufaika kutokana na elimu ambazo wamekuwa wakipeana kwa kuwashirikisha Wataalam mbalimbali
Rebeca Mdala ni mmoja wa Wanachama wa umoja huo na ambaye amekuwa akijihusisha na Biashara pamoja na kusaiia Watoto wanaoishi kwenye Mazingira magumu, amesema kutokana na kujengeana uwezo ambao wamekuwa wakiupata kupia kwenye umoja wao amefanikiwa kiutendaji katika shuguli zake kuihudumia jamii
Hafla hiyo sambamba na kufundwa na wataalam wa Saikolojia, kwa pamoja wametoa tuzo kwa Wanawake ambao wamekuwa wakifanya shughuli zao za kuhudumia jamii kwa werdi katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na Afya, Elimu, Ustawi wa Jamii na Wajasiriamali kwa kuwa mfano mzuri
Maoni
Chapisha Maoni