Watumiaji wa vyombo vya moto hususa waendesha Pikipiki wametakiwa kuhakikisha wanapata elimu ya usalama Barabarani wafahamu matumizi ya barabara ili waweze kuepuka au kupunguza ajali zisizo za lazima zinazogarimu maisha ya wananchi wengi
Watumiaji wa vyombo vya moto hususa waendesha Pikipiki
wametakiwa kuhakikisha wanapata elimu ya usalama Barabarani wafahamu matumizi ya barabara ili waweze kuepuka au kupunguza
ajali zisizo za lazima zinazogarimu maisha ya wananchi wengi
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa wilaya ya Kibondo
Mkoaani Kigoma, Luis Bura, aliyewakilishwa na katibu tawala wa wilaya hiyo Ayub
Sebabili alipo alikwa kama mgeni rasmi wakati wa kufunga mafunzo ya siku saba
ya waendesha Pikipiki maalufu kama Bodaboda wapatao 240 hafla iliyofanyika
Mjini kibondo
Alisema kuwa ajali nyingi zinazotokea kwa waendesha pikipiki
wengi ni kwa sababu ya ukosefu wa elimu ya barabarani kutokana na mtu kujifunza
kuendesha asubuhi na jioni kuanza kubeba abiria jambo ambalo ni hatari kwa
maisha ya watu kuwani Mtu huyo anakuwa hajajua namna ya kutumia
barabara, na kuwataka waendesha pikipiki
kufuata taratibu za usalama barabarani kwa kuacha kubeba abiria zaidi ya
mmoja
Awali waendesha Pikipiki
hao katika lisara yao walisema kuwa wanakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwa ni pamoja ukosefu wa leseni, baadhi na baadhi ya abiria
kukataa kuvaa kofia ngumu kuhofia maambukizi ya magonjwa ya ngozi hali
inayopelekea Askali wa usalama barabarani kuwakmata kwa makosa hayo na kuiomba
serikali kufanya utaratibu wa mapema ili wanapohitimu mafunzo hayo wapate
leseni
Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika lisilokuw la
kiserikali linalojihusisha na kutoa mafunzo ya ujasiliamali na kuondoa
umasikini Apec Repicius Timanywa ambae shirika lake ndilo lililosimamia mafunzo
hayo amewambia waendesha pikipiki hao
kuwa kupitia shirika lake leseni zao watafikishiwa katika maeneo yao ili
kuondoa usumbufu wa kutumia garama kubwa kufuata leseni
Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani Stephan Joka alitumia
nafasi hiyo kuwataka Madereva hao kufanya kazi zo kwa kutumia elimu waliyopewa,
na kusema kuwa ni vema kuhakikisha wanabadili umiliki wa vyombo hivyo vya moto
ili hata inapotokea kikaibiwa iwe laisi kukitafuta tofauti kuliko kuendelea
kubaki na umiliki wa mtu mwingine hatua inayosababisha usumbufu linapotokea
tatizo
Respius Timanywa Mkurugenzi Apec alipokuwa akiwahutubia mamia ya waendesha Pikipiki wakati wa ufugaji wa mafunzo mjini Kibondo mkoani kigoma |
Ayubu Sebabili katibu tawala W Kibondo aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo Luis Bura katika hafla fupi ya kufunga mafunzo ya waendesha Bodaboda |
Baadhi ya wahitimu hao ambao ni Thobias salvatory na Imara
Seleman wamepongeza uamuzi wa serikali kupitia shirika la Apec kuwafikishia mafunzo hao kwenye maeneo yao na
kueleza walikuwa wanafanya kazi kwa mazoea pasipo kujua jinsi ya kutumia
barabara unapokuwa unaendesha chombo cha moto
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni