Kibondo; Halmashauri ya wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma imepokea Magari mawili ya kubeba wagonjwa aina ya Toyota Land Cruiser yaliyotolewa na shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia Watoto Unicef ambapo magari hayo yanalenga kupunguza adha na kuokoa maisha ya wanawake wajawazito na watoto


Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri Wilaya kakonko Lusubilo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari baada ya makabidhiano ya magari ya kubeba wagonjwa yaliyotolewa na Unicef 

Magari ya kubeba wagonjwa yaliyotolewa na uncef


Fadhil Seleman baada ya kukabidhiwa Magari ya kubeba wagonjwa
Kibondo; Halmashauri ya wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma imepokea Magari mawili ya kubeba wagonjwa aina ya Toyota Land Cruiser yaliyotolewa na shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia Watoto Unicef ambapo magari hayo yanalenga kupunguza adha na kuokoa maisha ya wanawake wajawazito na watoto

Katika hafla ya makabidhiano  ya magari hayo, iliyofanyika jana mjini Kakonko, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Lusubilo Joel, alisema kuwa kutokana na adha wanazozipata wanawake wajawazito na watoto, shirika hilo la Unicef limetoa magari hayo kwa mkopo ambao utalipwa kwa muda wa miaka mitano na kuitaka idara ya afya ya wilaya hiyo kuyatumia kwa malengo mahususi ili yaweze kuleta tija

 Mkuu wa wilaya hiyoCanol Hosea Ndagala alipokuwa akikadidhi magari hayo kwa Mganga mkuu wa wilaya, Bw Seleman Faadhil ambapo   moja litatumika katika Kituo cha afya Kakonko ambacho kinatumika kama Hospital ya wilaya, na lingine litapelekwa katika kituo cha Nyanzige Tarafa ya nyaronga amesema kuwa ni vema utunzaji wa mali za umma ukatiliwa mkazo ili kuepuka hasara zisizokuwa za lazima

Aidha Canol Ndagala alisema pamoja na kupata nyenzo za kufanyia kazi ni vema na huduma bora zikapatikana ikiwa ni pamoja na lugha nzuri kwa wagonjwa mara wanapoitaji msaada kwa watumishi wa afya  huku kaimu mganga mkuu wa wilaya ya kakonko Selemani Fadhil akieleza matatizo waliyokuwa wakikumbana nayo kutokana na ukosefu wa gari la kubeba wagonjwa

‘’Kipindi kilichopita wananchi walikuwa wanapata shida sana kupata huduma za Afya lugha zisizokuwa rafiki, mara wanapofika kwenye vituo vya afya na Hospital hali iliyowafanya wengi kukata tamaa mambo hayo kwa kipindi hiki hatutegemei yawepo kila mtu afaye kazi kwa uadilifu kama taaluma yake inavyomuelekeza alisema Ndagala’’

Nao baadhi ya wananchi wamepongeza serikali ya Tanzania kwa kukubali kupokea mkopo huo na kueleza kuwa wanawake wamekuwa wakipata shida anapopatikana mgonjwa kutafuta usafiri wakati huo wengine wamekuwa wakisafirishwa kwa pikipiki hali ambayo ni hatari kwa mgonjwa husika

Muuguzi msaidizi katika wodi ya kituo cha Afya Kakonko, akina mama Beatrice Muyevu alisema kupatikana kwa magari hayo kutasadia kuondoa vifo vya watoto na wanawake kwa kuwa kutokana na jografia ya wilaya ya Kakonko alipokuwa akipatikana mgonjwa wengi walikuwa wanafika hospitalini watoto wakiwa wamefia tumboni na wanawake kupata shida kubwa 

Mwisho

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji