Kibondo;Kwakuwa Serikali ina lengo la kuinua na kuboresha viwango vya elimu hapa nchini kwa kutilia mkazo utengezaji wa Madawati, baadhi ya walimu hasa katika shule za msingi wameomba miundondo mbinu ya majengo nayo ipewe kipaumbele ikiwa ni pamoja na nyumba za walimu ili kuongeza moyo wa ufundishaji
Kibondo;Kwakuwa Serikali ina lengo la kuinua na kuboresha viwango vya elimu hapa nchini kwa kutilia mkazo utengezaji wa Madawati, baadhi ya walimu hasa katika shule za msingi wameomba miundondo mbinu ya majengo nayo ipewe kipaumbele ikiwa ni pamoja na nyumba za walimu ili kuongeza moyo wa ufundishaji
Baadhi ya walimu wilayani Kakonko Mkoani Kigoma wakiongea na Mwananchi jana mjini kakonko, ambao ni Theopister Balakebura na Prosper Methew walisema hivi sasa zipo changamoto nyingi katika shule hasa upungufu wa madasarasa wanafunzi kuzidi idadi inayotakiwa katika vyumba vya madarasa na walimu kukosa nyumba za kuishi hali inayosababisha ufuatiliaji wa wanafunzi kuwa mdogo
Akitoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo na utekelezaji wake Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Kakonko Lusubilo Joel alieleza kuwa mikakati inayofanywa na halmashauri yake kwa sasa licha ya kipato kidogo ni pamoja na kuongeza vyumba vya madarasa hata madawati yanayopatikana yapate pakuhifadhiwa na kujenga nyumba za walimu ili kuondoa usumbufu
Katika hatua nyingine halmashauri hiyo imepokea Madawati 200 yenye thamani tsh million 18 yaliyotolewa na shirika lisilo la kiserikali Social Action Trust Fund la Jijini Dar es Salaam ikiwa ni lengo lile lile la kuininua kiwango cha elimu na kuitikia wito wa Rais John Magufuli kama alivyosema Afisa mwandamizi wa shirika hilo Helena Chikamo ambapo aliwaomba wadau wa elimu kuendelea kujitoa ili kufikia malengo mahususi
Wakitoa shukran juu ya msahada huo wa madawati Juma Maganga mwenyekiti wa halmashauri ya Kakonko na Zainab Mbunda katibu Tawala walisema wanaendelea kutafuta wahisani kuziba pengo lililobaki kabla Agust 30 2016 , huku afisa elimu Christopher Bukombe akieleza upungufu waliokuwa nao hadi sasa ni 1688 na kuitaka jamii kuwa na tabia ya kuwelekeza watoto kutunza mali za umma yakiwemo Madawati mashuleni
''Kufikia hivi sasa uhaba tuliokuwa nao umeshuka sana tofauti na hapo awali maana tulikuwa na upungufu wa madawati 6000 lakini kufikia muda huda huu tunahitaji madawati 1688 alisema Juma Maganga mwenyekiti halmashauri Kakonko''
Baadhi ya Wajumbe waliudhuria hafla ya kukabhiwa Madawati katika halmashauri ya Kakonko |
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Maendeleo Kakonko wakiwa Darasani |
Madwati yaliyotolewa na shirika la Satf |
Juma Maganga mwenyekiti Halmashauri Kakonko |
Helena Chikomo Afisa Mwandamizi Satf alipokuwa akikabidhi madawati yaliyotolewa na shirika lake |
Lusubiro Joel Mkurugengenzi Mtendaji Kakonko |
Maoni
Chapisha Maoni