Kibondo;Wanafunzi wanaosoma katika shule binafsi wameeleza kukabiliwa na tatizo la walimu wanaopata ajira za muda katika shule zao na kisha kuondoka baada ya muda mfupi, kuwa hali hiyo inawahathiri kimasomo na kupelekea kushuka kwa kiwango cha elimu katika shule hizo tofauti na mategemeo yao




Lidia  ladislaus Mwanafunzi shule ya sekondari Bishop Mpango

Baadhi ya wanafunzi shule ya sekondari Mt Thomas More Kibogora


Jeremia Gwegenyeza makamu mwenyekiti
 CHAMA CHA WAMILIKI WA SHULE BINFSI 


WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI bISHOP mPANGO
 Kibondo;Wanafunzi wanaosoma katika shule binafsi wameeleza  kukabiliwa na tatizo la walimu wanaopata ajira za muda katika shule zao na kisha kuondoka baada ya muda mfupi, kuwa hali hiyo inawahathiri kimasomo na kupelekea kushuka kwa kiwango cha elimu katika shule hizo tofauti na mategemeo yao

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wanafunzi hao, ambao ni Peter Lyoba kutoka shule ya sekondari Kibogora iliyoko wilayani Kakonko, na Lidia Shija shule ya Sekondari Bishop Mpango ya wilayani Kibondo Mkoani Kigoma wamesema  kwakuwa kila mwalimu ana namna yake ufundishaji , hivyo wanapobadirishiwa walimu kila mara uwasababishia usumbufu kuanza upya kumuelewa

‘’Wakuu wengi wa shule binafsi wanategemea sana walimu wa muda amba wengi wao ukaa muda mfupi na kuondoka kutafuta ajira sehemu nyingine au wengine kwakuwa wanafunzi urudi masomoni kwa hali kile alichokuwa akikifundisha sicho atakachofundisha atakae kuja baadaealisema Lidia’’

Patric Mahinja ambae ni mkuu wa kituo cha Seminary ya Iterambogo, akijibu malalamiko ya wanafunzi hao, katika mahafali ya 10 kuhitimukidacho cha nne shule ya sekondari Kibogora, alisema kuwepo kwa walimu wa kudumu au wa muda si tatizo bali umuhimu ni kuwapata walimu ambao ni bora katika kazi zao na wenyekufanya kazi kwa weredi  kwa kuwafundisha wanafunzi

Hata hivyo baadhi ya walimu walisema sababu ziinazoyopelekea wengi wao kuhama au kuacha kazi kwenye shule binafsi baada ya muda mfupi ni kutokana na kutothaminiwa na waajiri wao hasa pale wanapopata matatizo hali inayopelekea kutafuata ajira serikalini ambako kuna usalama wa kazi licha ya mishahara mikubwa wanayopewa katika shule binafsi kama anavyoeleza Melesiana Leonidasi

Mwananchi iliamua kuzungumza na makamu mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa shule  na vyuo binafisi MOAF  hapa nchini, Jeremia Gwegenyeza ili kufahamu ni mikakati gani waliyonayo kuwasahawishi wamiliki wa shule hizo kutengeneza mazingira ili walimu wanaopatikana watulie katika vituo vya kazi wanameiomba serika kutoa uhuru wa ajira kama inavyotoa uhuru kwa maswala mengine juu ya elimu na kuongeza kuwa watu wengi licha ya kufundisha wanatafuta nafasi mbalimbali serikalini kama vile uafisa elimu uratibu nafasi ambazo hazipo katika sekta bianafsi

‘’Pia changamoto kubwa tuliyonayo ni garama kubwa ya kuwapata walimu kutoka nchi jirani za Kenya na Uganda ila tunajaribu kuishawishi serikali iliangalie hilo maana mtu mmoja kuja kufanya kazi hapa nchini garama ni dora 5000 kiasi ambacho ni kikubwa alisema Gwegenyeza’’

 Aidha Gwegenyeza aliongeza wao katika kutoa huduma za elimu wamewekeza fedha nyingi hivyo hawawezi kufanyakazi  kwa kuruhusu mambo yasiyofaha  hivyo pamoja na kutumia garama kubwa kuwapata walimu wa muda wako makini kuhakikisha ufundishaji unakuwa mzuri na kuwataka wanafunzi kutokuwa na mashaka
Mwisho

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji