Kakonko;Naibu waziri Ofisi ya Rais serikali za mitaa Tawala za mikoa Tamisemi Seleman Jafo amewataka wakuu wa Idara za halmashauri za wilaya kuhakikisha wanashirikiana na wafanyakazi walio chini yao katika utendaji kazi ili kuleta tija na kuondoa kukata tamaa kwa wafanyakazi
Kakonko;Naibu waziri Ofisi ya Rais serikali za mitaa Tawala za mikoa Tamisemi Seleman Jafo amewataka wakuu wa Idara za halmashauri za wilaya kuhakikisha wanashirikiana na wafanyakazi walio chini yao katika utendaji kazi ili kuleta tija na kuondoa kukata tamaa kwa wafanyakazi
Wito huo aliutoa jana alipokuwa akizungumza na Watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma katika ziara yake ya kutembelea baadhi ya mikoa na wilaya kukagua shuguli za maendeleo
Jafo alisema kumekuwepo na baadhi ya wakuu wa idara ambao hawana mausiano mazuri na wafanyakazi wa nchini yao hali inayopelekea wengi kukata tamaa ya kazi na kufanya shuguli za maendeleo ya kuwahudumia wananchi kutokuwa na mafanikio
‘’Kitu cha kusikitisha ni pale mfanyakazi anapoka muda mrefu bila kupandaraja huku wanaojiriwa nyuma yake wanapanda kisa hajatoa rushwa na rushwa mbaya zilizopo ni rushwa za ngono jamani wakuu wa idara watendeeni watu mema maafisa utumishi jipangeni vizuri kwa kusimamia idara zenu alisema Jafo’’
Katika hatua nyingine Mbunge wa jimbo la Muhambwe Kasuku Bilago alitumia nafasi hiyo kumuomba Naibu waziri huyo kuliangalia kwa umakini tatizo la ukosefu wa watumishi wa kada mbalimbali katika halmashauri ya kakonko jambo ambalo alilitaja kuwa ni changamoto kubwa
Ukosefu wa fedha za kuendeshea shuguli za kiofisi nalo ni tatizo kubwa kiutendaji katika halmashauri ya kakonko, kwani kazi zimekuwa zikikwama kufikia malengo kama Christopha Bukombe kaimu mkurugenzi mtendaji alivyomueleza naibu waziri huyo huku nae akimtoa wasiwasi kuwa taratibu zimshawekwa vizuri fedha zitaanza kutumwa kwenye halmashauri kikubwa ni matumizi mazuri
Kuhusiana swala la utawala bora kama naibu waziri Seleman Jafo alivyowataka watumishi wa halmashauri kushirikiana na kutendeana mema, mmoja wa watumishi walioshiriki katika kikao hicho Bi Azah Abdalah alisema hilo likiwepo katika maeneo ya kazi inakuwa ni shida japo yeye kwa kakonkohajakumbana nalo
Naibu waziri Jafo katika ziara yake wilayani Kakonko alitembelea baadhi ya shule za sekondari, Ujenzi wa Barabara zilizo chini ya halmashauri na Kituo cha afya Kakonko kinachotumika kama hospitali ya wilaya hiyo ambapo aliagiza uongozi uandike barua kwa ajili ya kujengewa Hospitali ya wilaya na kupongeza jinsi kazi zinavyoendeshwa kwa ujumla katika wilaya hiyo ikilinganishwa na uchanga wake
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni