Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2017

Kibondo:Jamii Taasisi mbalimbali Watu Binabfisi wanasiasa wametakiwa kulitazama kwa jicho la pekee swala la uchangiaji huduma za afya bila kujali na kuacha kuilalamikia serikali ili kuokoa maisha ya watu wanaokuwa wamekutana na magonjwa hasa kwa upande wanawake wajawazito na WatotoJ

Picha
Tumain Bilimana  Diwan viti maalum ICT Kibondo Juma Ramadhan Katibu Mwenezi ACT Kigoma Kibondo :Jamii Taasisi mbalimbali Watu Binabfisi wanasiasa wametakiwa kulitazama kwa jicho la pekee swala la uchangiaji huduma za afya bila kujali  na kuacha kuilalamikia serikali ili kuokoa maisha ya watu wanaokuwa wamekutana na  magonjwa  hasa kwa upande wanawake wajawazito na Watoto Uchakavu wa miundo mbinu, ukosefu wa Madawa na vifaa tiba na Nyumba za Watumishi ikiwemo umbali wa kufuata huduma za afya  ni changamoto kubwa hasa kwa wananchi wa hali ya chini hivyo ni vema jamii ikahamasishwa juu ya kujitolea  unachangiaji wa mifuko ya afya ya jamii na Bima ya afya ikilinganishwa na huduma zinazotolewa bure kwa Wazee, Watoto chini ya miaka tano na Wajawazito,   Akiongea jana Katibu mwenezi wa Chama ACT Wazalendo Mkoa wa Kigoma Juma Ramadhani wakati wa maadhimisho ya miaka 3 ya kuanzishwa kwa chama hicho yaliyofanyika Kimkoa kwa kutembelea Hospitali ya wilaya kibondo kwa ku

Kibondo;Baadhi ya walimu wa shule za msingi Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma, waliohamishwa vituo vipya vya kazi wameshindwa kufika katika vituo walikohamishiwa baada ya Halmashauri ya wilaya kushindwa kuwalipa stahiki zaoGabliel Chitupila Kaimu Mkurugenzi Kibondo

Picha
 Kibondo; Baadhi ya walimu wa shule za msingi  Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma, waliohamishwa vituo vipya vya kazi wameshindwa kufika katika vituo  walikohamishiwa baada ya Halmashauri ya wilaya kushindwa kuwalipa stahiki zao Wakiongea na gazeti ili jana, baadhi ya walimu hao amabo ni Anna Bakari aliyekuwa nafundisha shule ya Msingi  Kibondo nakuhamishiwa Kigendeka  na Anthon Sakala alikuwa vile Kibondo na kuhamishiwa shule ya Msingi Kahama walisema kuwa  walipewa barua za uhamisho tangu feb17mwaka huu, lakini hadi may11/2017 hawajalipwa pesa za usumbufu na za kusafirisha mizigo yao kama taratibu zinavyoelekeza badala yake wanaambiwa wajisafirishe wenyewe ‘’Kila tunapoenda kumuona mwajili wetu ili tupewe stahiki zetu, tunaambiwa tujisafirishe malipo yote baadae na hapa tuko mitaani na jambo ili si jema maana kanuni zinasema mfanyakazi anapohamishwa lazima alipwe pesa za usumbufu, na safari toka kwa mwajili’’ alisema Anthon Sakata hilo lilihamia katika baraza la Madiwani kwe

Msiba wa Kitaifa

Picha
Msiba wa Kitaifa Tunawapa pole wazazi ndugu na Jamaa wa wanafunzi waliokufa kwenye ajali ya Gari huko Karatu Msiba huu ni wetu wote huvyo tunamuomba Mungu awape uvumilivu wazazi wa karibu katika Kipindo hiki kigumu Katika hili kila mwanadamu mwenye akili timamu analo la kujifunza katika maisha yake anayoishi nayo msiba huu unatisha na unatia simanzi kumbwa mioyoni mwetu  kwani umewachukua watoto wadogo na kukatisha ndotro zao na malengo ya wazazi

Madiwani wa Chadema katika Baraza la halmashauri ya wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma juzi walimua kugoma kuendelea kushiriki kikao cha baraza hilo cha robo ya tatu wakidai kutotendewa haki kwa kwa kutojali hoja wanazozitoa katika vikao mbalimbali

Madiwani wa Chadema katika Baraza la halmashauri ya wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma juzi walimua kugoma kuendelea kushiriki kikao cha baraza hilo cha robo ya tatu  wakidai kutotendewa haki kwa kwa kutojali hoja wanazozitoa katika vikao mbalimbali Wakati wa kuanza mkutano huo, baada ya kumalizika kwa sala ya ufunguzi Madiwani hao 9 akiwemo Mbunge wa wa jimbo hilo anaetokana na chama hicho, walibaki wamesimama huku kila mmoja akiwa ameinua mikono yote juu hali iliyopelekea Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Juma Maganga kuwasikiliza Katibu wa Madiwani upande wa Chadema Medas Mahamile alpoanza kueleza kuwa wamekuwa wakitoa hoja mbalimbali hazifanyiwi kazi na wenyeviti wa vijiji wanaotokana na Chama hicho wamekuwa wakisimamishwa bila utaratibu hivyo bila kufanyiwa kazi kwa hoja zao hawako tayari kuendelea na kikao Mwenyekiti wa Kikao hicho Juma Maganga aliwajibu kuwa hoja wanazotoa kwa wakati huo hazina mashiko ila kama wana malalamiko yao wafute taratibumaana kama ni wenyeviti wa

Korea Kaskazini: Nani alimrukia Kim Jong-un?

Picha
Ni picha ya mwanamume aliyeruka na kuonekana kana kwamba anabebwa na kiongozi huyo alipokuwa anasherehekea ufanisi wa majaribio hayo.. Kim Jong-un bila shaka alionekana kuwa mwenye furaha isiyo na kifani. Lakini mbona mtu amrukie mgongoni kiongozi wa kiimla, na ni nani anaweza kuthubutu kufanya hivyo? Wachanganuzi wanasema mwanamume huyo hana umaarufu mkubwa katika siasa za Korea Kaskazini. Mwanamke maarufu zaidi Korea Kaskazini Korea Kaskazini 'yafanyia majaribio injini mpya ya kurusha roketi' Hata hivyo, inadhaniwa huenda alitekeleza mchango muhimu katika majaribio hayo ya injini, na kuna uwezekano mkubwa huenda aliwahi kukutana na kujumuika na Kim awali. Mchanganuzi wa masuala wa Korea Kaskazini Michael Madden anasema nembo za cheo kwenye sare yake zinaashiria kwamba ni afisa wa ngazi wa wastani katika kikosi cha Wanajeshi Maalum wa Angani wa Korea Kaskazini. Kikosi hicho ndicho husimamia makombora yanayotumiwa kutekeleza mashambulio nchini humo. Ingawa ku

Trump: Mpango wa afya, Obamacare wafikia tamati

Picha
Utawala wa Rais Donald Trump umekuwa ukishangilia baada ya Bunge la wawakilishi kupitisha muswada uliobatilisha mpango wa afya wa Obamacare ,sheria ya Obama kuhusu gharama nafuu za upatikanaji wa matibabu. Mpango huo wa huduma za afya wa Obama ulikuwa ukitoa huduma za bima ya afya kwa mamilioni ya raia wa Marekani, hivyo kutengua mpango huo ulikua moja ya ahadi ya Trump wakati wa Kampeni za urais. Muswada huo umepita kwa ushindi mwembamba wa kura 217 kwa 213. Muswada huo sasa utapelekwa kwenye bunge la Senate ambao walitoa wito wa kufanyika kwa mabadiliko ya sheria. Mwandishi wa BBC mjini Washington amesema muswada huo haujulikani utaathiri watu wangapi kutokana na kupoteza bima za afya. Akizungumza baada ya kupigwa kura, rais Trump ameseama ana uhakika muswada huo utapita kwenye bunge la Senate. '' kwa miaka miwili nimekuwa nikifanya kampeni na nawaambia kila nilipokuwa nikienda, watu walikuwa wakiathiriaka na mpango huu wa Obamacare, kwa kuwa mimi ninahusika kwe

Wakati Taifa likiwa katika mchakato wa kuwatambua na kuwaandikisha raia wake kwa ajili ya na kuwapatia vitambulisho, vya Uraia, wananchi hasa wakazi wa Mkoa wa Kigoma, wametakiwa kujitokeza na kuwatambua wahamiaji haramu ili kuepuka kukwamisha zoezi hilo

Picha
Emmanuel Maganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luis Bura Mkuu wa wilaya Kibondo Wakati Taifa likiwa katika mchakato wa kuwatambua na kuwaandikisha raia wake kwa ajili ya  na kuwapatia vitambulisho, vya Uraia, wananchi hasa wakazi wa Mkoa wa Kigoma, wametakiwa kujitokeza na kuwatambua wahamiaji haramu ili kuepuka kukwamisha zoezi hilo Akiongea na wananchi  wa maeneo mbalimbali ya wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma Mkuu wa Mkoa huo Brigedia General Mstaafu Emmanuel Maganga wakati  wa ziara yake akihamasishaji shuguli za maendeleo   amesema ikilinganishwa na jografia ya mkoa wa Kigoma wamo Raia wa Kigeni ambao wameingia nchini kinyume na Taratibu hivyo wasipowekwa wazi wanaweza kujiingiza katika zoezi hilo   Amewataka wale wote amabao si Laia wa Tanzania kutojiingiza katoka zoezi hilo  hata kama wao  wanadhani wamezaliwa hapa nchini maana hiyo si sababu ya kuwafanya kuwa watanzania   hata kama wamekaa muda mrefu ''Tunajua kwa ujanja na kutumia fedha mnaweza k