Kibondo;Baadhi ya walimu wa shule za msingi Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma, waliohamishwa vituo vipya vya kazi wameshindwa kufika katika vituo walikohamishiwa baada ya Halmashauri ya wilaya kushindwa kuwalipa stahiki zaoGabliel Chitupila Kaimu Mkurugenzi Kibondo
Kibondo;Baadhi ya walimu wa shule za
msingi Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma,
waliohamishwa vituo vipya vya kazi wameshindwa kufika katika vituo walikohamishiwa baada ya Halmashauri ya wilaya
kushindwa kuwalipa stahiki zao
Wakiongea na gazeti ili jana, baadhi ya walimu hao amabo ni
Anna Bakari aliyekuwa nafundisha shule ya Msingi Kibondo nakuhamishiwa Kigendeka na Anthon Sakala alikuwa vile Kibondo na
kuhamishiwa shule ya Msingi Kahama walisema kuwa walipewa barua za uhamisho tangu feb17mwaka
huu, lakini hadi may11/2017 hawajalipwa pesa za usumbufu na za kusafirisha
mizigo yao kama taratibu zinavyoelekeza badala yake wanaambiwa wajisafirishe
wenyewe
‘’Kila tunapoenda kumuona mwajili wetu ili tupewe stahiki
zetu, tunaambiwa tujisafirishe malipo yote baadae na hapa tuko mitaani na jambo
ili si jema maana kanuni zinasema mfanyakazi anapohamishwa lazima alipwe pesa
za usumbufu, na safari toka kwa mwajili’’ alisema Anthon
Sakata hilo lilihamia katika baraza la Madiwani kwenye kikao
cha robo ya tatu kilichofanyika jana ambapo Razalo Piter diwani kata ya Busunzu alitaka
kufahamu hatima ya walimu hao na wanafunzi mashuleni ambao awapati huduma za
masomo mashule kwa muda mrefu huku kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo Gabriel
Chitupila akidai atawachukulia hatua walimu wote ambao hawajaripoti vituon kwao
kwani walisha taarifiwa kuwa watalipwa
Simon Kanguye mwenyekiti wa halmashauri hiyo alimtaka
mkurugenzi kulitaza upya swala la
kuwahamisha walimu hao kwani linafanyika bila kuwepo bajeti ya kufanya hivyo na
nilazima walimu walipwe ili waende kwenye vituo vyao vya kazi
Alipotakiwa kueleza hali halis Katibu wa chama cha walimu
Kibondo Lyaki Majo alisema walimu wengi na wanashinda mitaani na kila wanapo
jaribu kudai upewa vitisho vya kufukuzwa kazi jambo ambalo ni kuwanyima haki huku mbunge wa Jimbo la Mhambwe Atashasta
Nditiyae akimtaka mkurugenzi kuwarudisha walimu watatu waliiosimamishwa kazi
Haiwezekani serikali inahangaika kutaka kuajili walimu huku
wengine wanafukuzwa bila utaratibu hili si jema bali zifuatwe taratibu za
kazi’’ alisema Nditiye
Galiel Chitupila kaimu Mkurugenzi |
Simon Kanguye mwenyekiti Hshauri Kibondo |
Ntilo Nzigu mwenyekiti cwt Kibondo |
Anna Bakari Mwalimu |
Anthon Sakala Mwalimu |
Atashasta Nditiye Mbunge Muhambwe |
Lyaki Majo Katibu Cwt Kibondo |
Mwenyekiti wa chama cha walimu kibondo Ntilio Nzigo alisema
kuwa hali hiyo inawahathili walimu kisaikolojia kwa kulingana na zoezi la
kuhakiki vyeti udhaniwa nao wamo ndani ya kundi la wafanyakazi waliogushi au
watumishi hewa na kulingana na idadi kubwa ya walimu 129 kuwa mitaani ni
kuathili hali ya taaluma mashuleni kwani wanafunzi hawafundishwi kwa siku hi
ambazo walimu wako mitaani
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni