Wakati Taifa likiwa katika mchakato wa kuwatambua na kuwaandikisha raia wake kwa ajili ya na kuwapatia vitambulisho, vya Uraia, wananchi hasa wakazi wa Mkoa wa Kigoma, wametakiwa kujitokeza na kuwatambua wahamiaji haramu ili kuepuka kukwamisha zoezi hilo
Emmanuel Maganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma |
Luis Bura Mkuu wa wilaya Kibondo |
Wakati Taifa likiwa katika mchakato wa kuwatambua na kuwaandikisha
raia wake kwa ajili ya na kuwapatia
vitambulisho, vya Uraia, wananchi hasa wakazi wa Mkoa wa Kigoma, wametakiwa
kujitokeza na kuwatambua wahamiaji haramu ili kuepuka kukwamisha zoezi hilo
Akiongea na wananchi
wa maeneo mbalimbali ya wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma Mkuu wa Mkoa huo
Brigedia General Mstaafu Emmanuel Maganga wakati wa ziara yake akihamasishaji shuguli za
maendeleo amesema ikilinganishwa na jografia ya mkoa wa
Kigoma wamo Raia wa Kigeni ambao wameingia nchini kinyume na Taratibu hivyo wasipowekwa
wazi wanaweza kujiingiza katika zoezi hilo
Amewataka wale wote amabao si Laia wa Tanzania kutojiingiza
katoka zoezi hilo hata kama wao wanadhani wamezaliwa hapa nchini maana hiyo si
sababu ya kuwafanya kuwa watanzania hata kama wamekaa muda mrefu
''Tunajua kwa ujanja na kutumia fedha mnaweza kutaka kuwa kwenye mpango huo ili nanyinyi muhesabike kama watanzania hilo haliwezekani bila kufuata taratibu za uraia hata kam mzazi wako mmoja ni mtranzia haitakusidia mpaka utakapo ukana uraia wa mzazi mmojawapo na atakegundulika hatua kali za kisheria zitachikuliwa dhidi yake '' alisema Maganga
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni