Kibondo:Jamii Taasisi mbalimbali Watu Binabfisi wanasiasa wametakiwa kulitazama kwa jicho la pekee swala la uchangiaji huduma za afya bila kujali na kuacha kuilalamikia serikali ili kuokoa maisha ya watu wanaokuwa wamekutana na magonjwa hasa kwa upande wanawake wajawazito na WatotoJ


Tumain Bilimana  Diwan viti maalum ICT Kibondo

Juma Ramadhan Katibu Mwenezi ACT Kigoma


Kibondo:Jamii Taasisi mbalimbali Watu Binabfisi wanasiasa wametakiwa kulitazama kwa jicho la pekee swala la uchangiaji huduma za afya bila kujali  na kuacha kuilalamikia serikali ili kuokoa maisha ya watu wanaokuwa wamekutana na  magonjwa  hasa kwa upande wanawake wajawazito na Watoto

Uchakavu wa miundo mbinu, ukosefu wa Madawa na vifaa tiba na Nyumba za Watumishi ikiwemo umbali wa kufuata huduma za afya  ni changamoto kubwa hasa kwa wananchi wa hali ya chini hivyo ni vema jamii ikahamasishwa juu ya kujitolea  unachangiaji wa mifuko ya afya ya jamii na Bima ya afya ikilinganishwa na huduma zinazotolewa bure kwa Wazee, Watoto chini ya miaka tano na Wajawazito,  

Akiongea jana Katibu mwenezi wa Chama ACT Wazalendo Mkoa wa Kigoma Juma Ramadhani wakati wa maadhimisho ya miaka 3 ya kuanzishwa kwa chama hicho yaliyofanyika Kimkoa kwa kutembelea Hospitali ya wilaya kibondo kwa kufanya usafi na kutoa vitu mbalimbali kwa wagonjwa na kueleza hali halisi waliyoiona hospitalini hapo hasa ukosefu wa damu

Hata hivyo baadhi ya wanachama wa chama hicho ambao ni tumain Bigilimana na Hosea Lameck walioshiriki katika maadhisho hayo walisesema pamoja na kufanya shuguli za usafi na kuwatembelea a  kwa ujumla uchangiaji huduma za afya ni jambo linalotakiwa kuelezwa kwa ufasaa kwenye  jamii  kwani linabeba roho na maisha ya watu

Hospitali nyingi Vituo vya afya na Zahanati hapa nchini hali si nzuri kwani hata watumishi wanaishi katika mazingira ambayo si rafiki kwa kukosa nyumba za kuishi na ni jukumu la maeneo husika kuanza kwa hatua za wali ili serikali uamalie kwa upande wake kwa hiyo jama jamii husika haitaelimishwa tutabaki palepale na malalamiko hatayataisha’’alisema Bilimana

Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Adam Jonathan aliyapongeza makundi yanayofika hospitalini hapo kwa ajili ya kujitolea kufanya kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa damu na kuwatembelea wagonjwa na kuwafariji wasiyojiweza kwa kutoa vitu

Nao baadhi ya wagonjwa na wasidizi waliotembelewa na wanachama wa ACT Wazelendo katika Hospitali ya wilaya kibondo katika maadhimisho walishukuru zawadi walizopewa ambapo vitu vilivyolewa ni  vitu vyenye Thamani ya tsh laki saba na 50 elf ikiwa ni sabuni za kufulia na kuogea, powder na mafuta ya kupaka kwa ajili ya watoto na dawa za meno
Mwisho

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji