Madiwani wa Chadema katika Baraza la halmashauri ya wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma juzi walimua kugoma kuendelea kushiriki kikao cha baraza hilo cha robo ya tatu wakidai kutotendewa haki kwa kwa kutojali hoja wanazozitoa katika vikao mbalimbali

Madiwani wa Chadema katika Baraza la halmashauri ya wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma juzi walimua kugoma kuendelea kushiriki kikao cha baraza hilo cha robo ya tatu  wakidai kutotendewa haki kwa kwa kutojali hoja wanazozitoa katika vikao mbalimbali

Wakati wa kuanza mkutano huo, baada ya kumalizika kwa sala ya ufunguzi Madiwani hao 9 akiwemo Mbunge wa wa jimbo hilo anaetokana na chama hicho, walibaki wamesimama huku kila mmoja akiwa ameinua mikono yote juu hali iliyopelekea Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Juma Maganga kuwasikiliza

Katibu wa Madiwani upande wa Chadema Medas Mahamile alpoanza kueleza kuwa wamekuwa wakitoa hoja mbalimbali hazifanyiwi kazi na wenyeviti wa vijiji wanaotokana na Chama hicho wamekuwa wakisimamishwa bila utaratibu hivyo bila kufanyiwa kazi kwa hoja zao hawako tayari kuendelea na kikao

Mwenyekiti wa Kikao hicho Juma Maganga aliwajibu kuwa hoja wanazotoa kwa wakati huo hazina mashiko ila kama wana malalamiko yao wafute taratibumaana kama ni wenyeviti wa vjiji kusimamishwa kazi wanatakiwa wakate rufaa kwa mkuu wa mkoa mambo yafuatiliwe kwa mujibu wa sheria, hatua iliyowasababisha kuamua kuondoka ndani ya mkutano kwa kukataa kushiriki 

‘’Hatuwezi kuendelea na kikao kwa sababu sisi hatuna sauti ndani ya Baraza hilo kwa sababu ya kutukandamiza hasa tunapotoa hoja mbalimbali tunapokuwa kwenye vikao hivyo tunawaacha waendelee wenyewe’’ alisema Medas  

Hata hivyo Mwenyekiti huyo aliwataka kuacha tabia ya kutafuta umaalufu wa kisiasa kwa njia ya namna hiyo bali wanatakiwa kutambua kuwa walichaguliwa na wananchi ili wawakilishe matatizo yao wanaposusia wanakuwa awawatendei haki wananchi wao

Mbunge wa Jimbo la Buyungu Kasuku Bilago alisema kumekuwepo na hali ambayo madiwani wa chadema wameshindwa kuvumilia kwani wamekuwa wakitoa hoja au ushauri mara wanaposoma makablasha wanakuta wameandikwa watu wengine kama mkuu wa wilaya kuwa ndo wametoa hoja hizo yakiwemo mambo mengine mengi

Baraza hilo lenye jumla ya Madiwani 19 Ccm 10 na Chama cha demokrasia na maendeleo  madiwani 9 kilibaki na idadi 10 tu wanaoongozwa na ccm baada ya chadema kususia 
Mwisho     

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji