Morogoro;Takwimu zinaonyeshaTanzania bado inakabiliwa na kiwango cha juu cha ukatili wa kijinsia ikiwemo ndoa na mimba za utotoni, pamoja na vipigo kwa wanawake kutoka kwa waume zao licha ya juhudi mbali mbali za kupinga hatua hiyo na sheria kali kutungwa bado matukio ya aina hii yanazidi kuongezeka.
Morogoro;Takwimu
zinaonyeshaTanzania bado inakabiliwa na kiwango cha juu cha ukatili wa kijinsia
ikiwemo ndoa na mimba za utotoni, pamoja na vipigo kwa wanawake kutoka kwa
waume zao licha ya juhudi mbali mbali za kupinga hatua hiyo na sheria kali
kutungwa bado matukio ya aina hii yanazidi kuongezeka.
Utafiti wa hali ya afya ya
uzazi,mtoto na malaria wa mwaka 2015/2016 unaonesha kuwa idadi ya wasichana
wanaopata watoto katika umri wa miaka 15-19 imeongezeka mpaka kufikia asilimia
27 mwaka 2015 kutoka asilimia 23 mwaka 2016
Vitendo vya ukatili wa kijinsia hapa nchini vinatajwa
kuendelea kuwepo licha ya juhudi nyingi za kupiga vita vitendo hivyo kutiliwa
mkazo ikiwa ni pamoja na mashirika mbalimbali na serikalia kwa ujumla hasa
kusababishwa na uelewa mdogo katika jamii kufichua vitendo hivyo
Baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa licha
kuendelea kuwepo kwa vitendo hivyo, Tanzania bado iko katika nafasi nzuri ya
kupiga vita ukatili huo katika bara la Afrika ikilinganishwa na mataifa mengi
ya bara la Afrika. Imeshika nafasi ya 6 zaidi ya mataifa ya Lesotho,
Msumbiji, Togo, Afrika Kusini na
Namibia.
Makundi mbalimbali wakiwemo wanahabari wametakiwa kuendelea
kutoa elimu katika jamii, kauli hiyo imetolewa na mkufunzi wa maswala ya
kijinsia Agnes Kabigi katika mafunzo na waandishi wa habari ya kujenga uelewa
juu kupinga ukatitili huo yanayofanyika mjini Morogoro
Kabigi alisema kwa kuwa Wanahabari nao ni sehemu ya jamii
inawapasa kupaza seuti za wanyonge ili kufikia malengo yanayokusudiwa kwani
hali ukatili huo bado upo na umekuwa ukuripotiwa japo kwa kiwango cha chini
huku baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo Ambao ni Seny Emmanuel na Mwajuma
Mmanga walisema, ili kufikia malengo ni vema ushirikiano ukawepo kwa makundi
husika na sheria ikafuata mkondo
‘’Licha ya kuonekana kuwekwa
wazi badhi ya matukio, bado hali haijawa nzuri kwani vitendo vya
unyanyasaji wa kijinsia viaendelea kushamili katika baadhi ya maeneo hapa
nchini na vingi haviripowi kutokana na changamoto mbalimbali zinazoyakabili
makundi tofauti ikiwemo ukiwemo ukandamizaji ‘’ alisema Kabigi
Hata hivyo kwa upande wao baadhi wakazi wa Mji wa Morogo
ambao ni Frola Poul na Emmanuel Wilson, walisema kuwa mfumo dume mitazamo ya
baadhi ya watu na kukwepa majukumu imekuwa nisababu ya wanawake na Wanaume
kukosa haki zao
''Wanaonyanyswa si wanawake pekee kama inavyofikiriwa na Watu
wengi hata wanaume katika Familia wapo wanaokosa haki za kimsingi nao migawanyo
ya majukumu kwa upande wao haijawa sawa kikubwa ni kuelimishana ili kubadili
Tabia na mitazamo inayotokana na hulkaka mbalimbali kama malezi, Makabila na
Uelewa Mdogo’’ alisema Wilson.
Maoni
Chapisha Maoni