Tatizo la ugonjwa wa Malaria linaloonekana kuwa moja ya sabababu za kupunguza nguvu kazi ya Taifa jamii imetakiwa kushirikiana bega kwa bega na serikali ili kuutokomeza ugonjwa huo hasa kwa kuharibu maeneo ya mazalia ya Mbu na katika makazi ya watu

Mkuu  wa wilaya ya Kibondo Luis Bura akinyunyizia dawa ya kuuwa Vimelea vya Malaria katika Bwawa kufugia samaki katika Kijiji cha Biturana

Juma Mnwele mkurugenzi Halmashauri ya Kibondo



Raya Chamabali mratibu Kitengo cha Malaria W Kibondo



Tatizo la ugonjwa wa Malaria linaloonekana kuwa moja ya sabababu za kupunguza nguvu kazi ya Taifa jamii imetakiwa kushirikiana bega kwa bega na serikali ili kuutokomeza ugonjwa huo hasa kwa kuharibu maeneo ya mazalia ya Mbu na katika makazi ya watu

Takwimu za  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto zinaonyesha hali ya maambukizi na vifo vitokanavyo na ugonjwa wa malaria imepungua kutoka asilimia 90 ya maeneo yenye mbu  hadi kufikia  asilimia 50  ya walioambukizwa  malaria tangu 2000 hadi 2017.

Aidha takwimu hizo zimebainisha kuwa, mikoa ya kanda ya ziwa ikiwemo Kagera na Geita  na mikoa ya Nyanda za juu Kusini ambayo ni Mtwara na Lindi ndiyo inayoongoza kwa maambukizi pamoja na idadi ya vifo kwa zaidi ya asilimia 50 toka mwaka 2008 hadi 2016.

Kwa upande wa mkoa wa Kigoma hali ya maambukizi ya  ugonjwa huo ni asilimia 38 ambapo walaya za kibondo na kakonko zinatajwa kuwa na maambukizi  zaidi ya wilaya zote za mkoa huo alieleza Mratibu wa Kitengo cha Malaria Wilayani Kibondo   Dk Raya Chambali, wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kunyunyizia Dawa ya Viuwa na dudu kwenye  madimbwi na Mabwawa yaliyo karibu na Makazi ya Watu iliyofanyika juzi kiwilaya katika Kijiji cha Biturana ambapo alisema kuwa ugonjwa huo umekuwa ukiathili zaidi watoto chini ya miaka mitano na wajawazito

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Kibondo Luis Bura aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo alisema licha ya kunyunyizia dawa hiyo bado jamii inatakiwa kuendelea kutumia njia zingine za kujikinga na ugonjwa huo kama kutumia vyandarua vyenye viatilifu

Nao baadhi ya wananchi waliohudhulia katika zoezi hilo, ambao ni Andrea Simon na Sofia Faida  walisema  kampeni itasaidia sana kwani watu wata watapata elimu ya kujikinga na maambukizi kwa kuwa ugonjwa huo umekuwa ukisababisha hasra kubwa kwa jamii kwa kutumia garama kubwa na kushindwa kufanya shughuli za uzalishaji mali

Kutokana na jitiada za serikali kupambana na ugonjwa huo, imetoa dawa hiyo ya kuuwa vimelea hivyo kwa halmashauri ya kibondo na imezitaka halmashauri kuendelea  kuhamasisha  umma juu ya  ufahamu wa ugonjwa wa malaria kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria. Elimu inatolewa juu ya matumizi sahihi ya vyandarua vyenye viuatilifu, kuhifadhi mazingira pamoja na kuijengea uwezo, kuiwezesha na kuisaidia mikoa na halmashauri ili, kupambana na malaria hapa nchini.


Mwisho

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao