Kibondo;Uelewa mdogo kwa baadhi ya wananchi juu ya rushwa ni moja changamoto zinazoikabili taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa

Kibondo;Uelewa mdogo kwa baadhi ya wananchi juu ya rushwa ni moja changamoto zinazoikabili taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa

Wananchi wengihawako tayari kutoa ushahidi pale wanapohitajika kufanya hivyo licha ya kuwa na taaria za kuwepo kwa watu  wenyekujihusisha na mambo ya rushwa halambayo ina sababisha kukwama kwa au kuchelewa kwa kesi

Akiongea juzi katika Tamasha lililoandaliwa kwa ajili ya kutoa elimu kwa jamii juu ya maswala ya Rushwa iliyofanyika katika kata ya mabamba wilayani Kibondo mkoani Kigoma  Kamanda wa Takukuru Michael Oyombe wilayani humo  alisema jamii nyingi hasa vijijini hawatoi taarifa katika vyombo husika pale wanapoona kuna viashiria vya rushwa na kueleza kuwa mpango huo niendelevu ili kutoa elimu kwa wananchi

Oyombe alisema hivi sasa zipo kesi mbili katika mahakama ya wilaya hiyo ambazo zinawakabili watu toauti kutokana na vitendo vya rushwa na kuitaka jamii kukataa kurubuniwa na watu kwa ajili ya kuahidiwa edha na vitu kwa ajili ya kuhujumu mali au vinginevyo

Hata hivyo baadhi ya wananchiwaliyohudhulia mkutano huo, ambao ni Mariether Jacob na Poul Mahwela  walisema wengi wao licha ya kutokuwa na uelewa wa vitendo vya rushwa uhofia kupata matatizo kutoka kwa wanaoonekana kuwa na viashilia vya ulaji rushwa

‘’Wengi tunahoia maisha yetu maana mwananchi wa kaaida mimi ninavyoikiri hawezi kula rushwa ila ni watu wenye uwezo sasa mimi nitawezaje kupambana na watu kama hao ‘’ alisema Marietheri

Aidha waliongezaa wanaothilika na tatizo hilo ni wananchi wa chini kabisha na kuiomba serikali kuzisimamia taasisi zake wakiwemo watumishi wake wanaoaminiwa na kupewa kazi mbalimbali kufuata utaratibu wa kisheria
Mwisho
Wakazi wa Mabamba Kibondo



Kleus Komwendo Oisa wa Takukuru Kibondo



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao