Vijana wanaohitimu mafunzo ya kishi hapa nchini wametakiwa kuzingatia viapo vyao kwa kuyatumia kwa usahihi mafunzo na ujuzi walioupata ili kutimiza hadhima ya serikali ya kuanzisha jesi la kujenga Taifa
Vijana wa Kikosi cha 824 kanembwa jkt wakiwa kwenye Gwaride wakati wakufunga mafunzo ya awali ya Kijeshi Op Meleran 2018 |
Vijana wa Kikosi cha 824 kanembwa jkt wakiwa kwenye Gwaride wakati wakufunga mafunzo ya awali ya Kijeshi Op Meleran 2018 |
Julias Kadawi mwakilishi wa Mkuu wa jkt Tanzania wakati kufunga mafuzo ya kijeshi Jkt Kanembwa |
Luis Peter Bura, Mkuu wa Wilaya Kibondo aliyekuwa mgeni rasmi katika kufunga mafunzo ya awali Jkt Kanembwa alipokuwa akiwahutubia Vijana wahitimu |
Luthen Kanal Mkuu wa Kikosi 824 Kanembwa |
Nazael Eliya akisoma lisara ya Wahitimu wa Mafunzo ya Kijeshi Jkt Kanembwa |
Vijana wanaohitimu mafunzo ya kishi hapa nchini wametakiwa kuzingatia viapo vyao kwa kuyatumia kwa usahihi mafunzo na ujuzi walioupata ili kutimiza hadhima ya serikali ya kuanzisha jesi la kujenga Taifa
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma Luis Bura aliyekuwa mgeni rasmi jana wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi Oparation Meleran katika kikosi cha 824 kj Kanembwa JKT ambapo alisema watakaporudi katika jamii kuungana na wananchi wengine katika shuguli za ujenzi wataifa wasihusishe na vitendo viovu bali wajikite katika kujishulisa na uzalishaji mali na ulinzi wa taifa
Nae mwakilishi wa mkuu wa jkt Tanzania Julias Kidawi, alisema hivi sasa vijana wa Tanzania wanakabiliwa na tatizo la mmommonyoko wa maadili kwa kuiga Tamaduni na mila zisizofaa za kutoka mataifa ya nje lakini Jkt imekuwa mstari wa mbele katika kuwaelekeza vijana katika malezi na kujitambua ili wafuate destuli za Tanzania zilizo njema
''Hali hiyo ya mmommonyoko wa maadili kwa vijana ni tatizo kuwa katika jamii zetu wengi wao kupoteza maisha wengine kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa kujiingiza katika vitendo vya matumizi ya madawa ya kulevya ngono nzembe ujambazi na mambo mengi mabaya na kupelekea kupoteza nguvu kazi ya Taifa'' alisema Kadawi
Vijana hao wapatao 732 waliobahatika kuhitimu mafunzo katika lisara yao iliyosomwa na Nazael Eliya wameahidi kutumia ipasavyo ujuzi walioupata, na kufuata taratibu za nchi kama miongozo inavyoelekeza huku Mkuu wa Kikosi hicho Luthen Kanal Amos Morro akisema licha ya vijana hao kufjifunza maswala ya ulinzi wamejifunza namna ya kuzalisha mali na maaadili
Wahitimu hao walianza mafunzo January 22 /2018 wakiwa vijana 739 lakini wenzao 7 walishindwa kumaliza kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na utovu wa nidhamu, kusistisha mkataba na kifo cha mtu mmoja hali iliyopelekea kuhitimu wakiwa idadi ya 732
Maoni
Chapisha Maoni