FPCT NYAWELA WAZINDUA JENGO JIPYA
Kanisa la Free Pentekote Tanzania FPCT Kibondo Mkoani Kigoma limefanya uzinduzi wa Jengo la Kanisa Jipya katika Mtaa wa Boma Nyawela, ambalo ujenzi wake ulilianza ujenzi wake mwaka 2021 na linatarajia kukamilika mwaka huu 2023
Akizindua Jengo la Kanisa hisa hilo Askofu wa Kanisa la FPCT Meshak Buhimbi amewapongeza Wahumini wa Kanisa hilo kujitolea Michango yao na kuhakikisha wanafanikisha malengo yao huku akiwataka kuendelea kujitoa kwa kazi zingingine za kijamii na kuwasaidia wahitaji
Akiwa katika Ibada ya kuadhimisha siku hii ya Pasaka Jamii imehaswa kushirikiana na serikali kupinga Vitendo viovu ili kudumisha Amani ya nchi kama anavyoeleza Askofu kanisa la Free pentekoste Kibondo Meshack Buhini katika Ibada iliyofanyika Kanisa la Nyawela Kibondo ambapo amesema licha ya uwepo wa sheria ipo haja ya Watu kujiepusha na uharifu kwa hiali yakiwemo mapenzi ya jinsia moja
Aidha meshak amesema licha ya uharibifu mkubwa unaonekana kutokana na mmomonyoko wa maadili ndani ya jamii Wakristo hawatakiwi kukata tamaa bali wawaeleze wenzao yakiwemo malezi bora kwa Watoto wao na kukataa uovu wa kila aina vikiwemo Vitendo vya Ushoga kwani ni Kinyume cha Maadili na Mila za Afrika na Tanzania
Nao baadhi ya Vijana ambao ni Wahumini wa Kanisa hilo, Nelson Malaki na Diana Jackson wamesema mmomonyoko wa maadili umekuwa ukichangiwa na baadhi ya wazazi kutokaa na Watoto wao na kuwaelekeza yanayowapasa kutenda badala yake muda wote wako katika masuala ya kutafuta fedha
''Tunaiomba jamii na serikali waendelee kutoa elimu za makuzi kwa Vijana na matumizi mazuri ya mitandao ambayo inatajwa kutumika Vibaya na wazazi watenge muda wa kuzungumza na Watoto wao namna ya kuishi kwa maadilihasa kwa makundi ya Vijana alaisema Diana
Nelson Malaki Mhumini |
Diana Jackson Mhuumini |
Meshack Buhimbi Askofu Kanisa la FPCT KIBONDO |
Askofu Buhimbi akikata utepe wakati akizindua Jengo la Kanisa la FPCT Nyawela |
Maoni
Chapisha Maoni