WANAFUNZI WASHINDWA KUFIKA SHULENI BAADA YA KUKUTA MTO UMEFURIKA
Baada ya kufungua shule kwa kumaliza likizo ya robo mwaka Wanafunzi wa shule ya sekondari Ikambi iliyoko Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma wameshindwa kufika shuleni hapo kuanza masomo baada ya kufika njiani na kukuta Mto umerika Maji na kushindwa kupita
Wanafunzi hao baadhi ambao ni Leonida Eduad na Jayros Yora wamesema Maji katika eneo hilo yamefunika Daraja ambalo huwa wanalitumia kuvu
ka kwenda shuleni kwao hivyo wameshindwa kuvuka kwa hofia kuzama
Mto huo Muwazi ulioko kwenye Kijiji cha Itumbiko umesababisha kukatika kwa mawasiliano ya shule ya Sekondari Ikambi na maeneo iirani ambapo wanafuni wa shule hiyo wameiomba serikali kurekebisha Miundombinu ya Barabara mawasiliano yarejee tena
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo imefika kwenye eneo la Tukio ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Evance Malasa amesema mpaka sasa hakuna madhala ambayo yameshatokea kutokana na Mtuo huo kujaa Maji na kuiomba serikali kujenga daraja lenye uwezo wa kuimili nguvu ya maji eneo hilo
Amesema kwa wamezuia Wananchi wanaojaribu kuvuka kwa Miguu kuacha kufanya hivyo ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza huku Meneja wa Tarura Wilaya ya Kakonko John Ambluce akisema wanafanya Tathimini ya haraka kwa ajili ya suluhisho la kudumu
Hata hivyo Malasa amesema amemwagiza Afisa elimu shule za sekondari kufanya utaratibu Wanafunzi hao 203 wapelekwe shule zingine kwa muda na sasa watahamishiwa kwa muda katika shule ya sekondari Kakonko wakati ujenzi ukifanyika kurudisha mawasiliano kwani eneo hilo ndilo wanalolitumia Wakulima wengi wa Mji wa Kakonko na Vijiji jirani
Imedaiwakulingana na Mvua zinazoendelea kunyesha, ndiyochanzo kikubwa cha kufurika Mto huo kwa Maji mengi yanatokea Nchini Burundi na kutiririkia Kakonko hata kama Mvua ni za wastani upande wa Kakonko
Kanali Evance Malasa Mkuu wa Wilaya ya Kakonko alipokuwa ametembelea eneo la Tukio Mto Muwazi |
Saamoja Ndilaliha Mwenyekiti Ccm Kakonko |
John Ablus Meneja wa Tarura W Kakonko |
Maoni
Chapisha Maoni