Serikali kuboresha Kilimo biashara
Baadhi ya washiriki waliohudhuria Kakikao kwa ajili ya kutoa na kupokea maelekezo ya serikali namna ya kununua na kuuza mazao ya Kilimo Kilichofanyika ukumbi wa Mikutano Mjini Kibondo Mkoani Kigoma Na Muhingo Mwemezi Kibondo Serikali ili kuboresha sekta ya Kilimo kwa kulenga kumuinua Mkulima imeweka utaratibu maalumu wa kuwasajili Wafanyabiashara wa Mazao wa ndani ya Nchi kusajili Vituo vya mauzo na wamiliki wa Mgala yanayohifadhi Mazao Gabriel Chitupila ambae ni Mkuu wa Idara ya Kilimo na Mifugo Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma alipokuwa akitoa ufafanuzi wa mpango wa serikali kwa wafanyabiashara wa Mazao, Wamiliki wa Magala, Watendaji wa Vijiji Kata na Maafisa ugani amesema kwa sasa Wakulima hawatafuatwa Mashambani na wafanyabiashara bali watauza Mazao yao kwenye Vituo maalum Wafanyabiashara watakuwa wananunua Mazao kutoka kwa wakulima baada ya kufikishwa kwenye Vituo vilivyosajiliwa kisha wafanyabiashara wa ndani watakuwa wanawauzia wenzao kutoka nje ya nchi badala y...