Burundi waomba Tanzania ushirikiano Mafunzo vyuo vya Uuguzi yaendelee kwa ajili ya kuboresha Taaluma
Proches Kitaronja Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kibondo alipokuwa akiongea na Wageni toka Nchini Burundi Katika Chuo cha Uuguzi Kibondo |
Habyalimana Juve Mkuu wa Chuo cha Uuguzi Gisulu |
alfreda Ndungulu Mkuu wa Chuo cha Uuguzi kIBONDO |
Burundi waomba Tanzania
ushirikiano Mafunzo vyuo vya Uuguzi yaendelee kwa ajili ya kuboresha Taaluma
Chuo cha Uuguzi Gisulu Mkoa wa Chankuzo Nchini Burundi kimeomba ushirikiano wa pamoja katika kubadilishana uzoefu wa mafunzo ya uuguzi kwa Wanafunzi wan chi hizi mbili
Wakiwa katika ziara ya mafunzo Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma Nchini Tanzania, wanafunzi na walimu kutoka Chuo cha uuguzi Gisulu Mkoani Chankuzo Burundi, wamesema licha ya Mitaala tofauti katika nchi zao, yapo mambo ambayo yakifanyika kwa kubadilishana uzoefu yaweza kuleta matokeo chanya na kuboresha taaluma hiyo
Habyalimana Juve Mkuu wa Chuo cha Uuguzi Gizulu amesema wameweza kuona utofauti uliopo katika Vyumba na Vifaa vya kujifunzia kwa njia ya matendo ambapo kwao hutumia chumba Kimoja wakati wenzao wa Tanzania wanatumia Vyumba kumi na Viwili hatua ambayo wamesema inaondoa changamoto ya ujifunzaji na kuongeza kuwa kwa Burundi Wanafunzi wanatumia muda wa miaka mitatu wakati Tanzania ni miaka minne
Ziara hiyo ya mafunzo Wanafunzi wameleeza tofauti wazoziona katika ujifunzji na namna wagonjwa wanavyopokelewa katika Vituo vya kutolea huduma za afya huku wito kwa Vijana watanzania wakitakiwa kuendelea kujivunia taaluma ya uuguzi kwani ni ya Kimatafa anaeleza Alfreda Ndungulu Mkuu wa chuo cha uuguzi Kibondo
Awali ujumbe wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kibondo uliotolewa na mwakilishi wa ofisi hiyo, Proches Kitaronja, umewataka Vijana kupenda kujifunza zaidi kwani mambo mengi yamekuwa yakibadilika kuendana na Teknolojia na kusistiza kudumisha mahusiano yalipo kati ya Tanzania na Burundi kwa kuwaendzi wahasisi wan chi hizi mbili kwa kudumisha amani na upendo
Maoni
Chapisha Maoni