WANAFUNZI WAIPONGEZA SERIKALI KUWAEPUSHIA KUTEMBEA MWENDO MREFU KM 10 KUFUATA ELIMU

 



Wanafunzi Shule ya sekondari Mkabuye waliohama kutoka Itaba Sekondari baada ya kujengewa shule kwenye Kata yao


Kibondo.Wanafunzi wa shule ya sekondari Mkabuye iliyoko Kibondo Mkoani Kigoma, wameipongeza serikali kuwajengea shule kwenye Kata yao ambayo imeanza kutoa huduma mwaka huu 2023 kwani hapo awali walikuwa wanatembea kilomita 10 kufuta huduma ya Elimu kwenye Kata nyingine ya Itaba

Baadhi ya Wanafunzi hao ambao ni Jonas Stanslaus na Sikitu Moses wamesema hali hiyo imekuwa ikiwasababishia usumbufu Mkubwa hasa katika masuala ya ujifunzaji ambapo taalauma imekuwa ikiporomoka kila uchao lakini kwa sasa adha hiyo imeondoka na wanapata elimu bila usumbufu

''Kama sisi Watoto wa Kike tumekuwa tukipata shida sana kutokana na mambo mengi yanayotukabili na wengine wenzetu waliacha masomo kutokana na umbali na tunapofika majumbani kazi zinatusubiri wakati huo tumechoka sana hali ambayo imekuwa ikipelekea wengi kuta Tamaa lakini kwa sasa tutasoma kwa bidiii kwakuwa tumejengewa shule karibu kwenye Kata yetu amesema Sikitu''

Akiwa kwenye Mkutano wa hadhala uliofanyika kwenye Kata ya Mkabuye Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Frolence Samizi amesema kulingana na uhitaji ulioko katika shule hiyo upungufu wa vyumba vya Madarasa na Maabara, serikali imetoa Shilingi Milion 600 ili kukamilisha miundombinu shuleni hapo kwani vyumba vilivyopo ni vitano na vitakavyoongezeka ni vyumba  vinane

Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo katika shukrani zake amesema kwa mwaka 2020/23 shilingi milion 204 zimepokelewa kwa ajili ya Miradi mbalimbali ya maendeleo vikiwemo vyumba vitano vya shule ya Sekondari Mkabuye vilivyojengwa kwa thamani shilingi mil 100

Pamoja na mambo mengine kwenye Mkutano huo wananchi wametoa kero zao zinazowakabili katika maeneo yao ikiwa ni upatikanaji wa msaada kwa Wanafunzi walioshindwa kuendelea na masomo Vyuo vya Kati na upatikanaji wa Pembejeo za Kilimo huku mbunge huyo akieleza kuwa kwa msimu huu wa kilimo changamo ya pembejeo haitakuwa kubwa kutokana na serikali kuleta Mbolea ya Luzuku Mapemakupitia Wakala wake

''Tunafahamu mwaka jana wakulima walihangaika sana kupata Mbolea hivyo sekali ililiona hilo ndiyo maana pembejeo zimefika mapema kupitia wakala anayeitwa Plani Nzugulu hivyo wananchi wanaweza kuanza kwenda kukunua mbolea pia Wakala huyo anataraji kuweka Kituo kingine cha uuzaji katika Kata ya Nyaruyoba kupunguza usumbufu kwa wakulima ''alisema Frolence Mbunge 




Frolence Samizi Mbunge wa Jimbo la Muhambwe akiwahutubia Wananchi Kata ya Mkabuye





Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji