Serikali kuboresha Kilimo biashara

 

Baadhi ya washiriki waliohudhuria Kakikao kwa ajili ya kutoa na kupokea maelekezo ya serikali namna ya kununua na kuuza mazao ya Kilimo Kilichofanyika ukumbi wa Mikutano Mjini Kibondo Mkoani Kigoma




Na Muhingo Mwemezi Kibondo


Serikali  ili kuboresha sekta ya Kilimo kwa kulenga kumuinua Mkulima imeweka utaratibu maalumu wa kuwasajili Wafanyabiashara wa Mazao wa ndani ya Nchi kusajili Vituo vya mauzo na wamiliki wa Mgala yanayohifadhi Mazao

Gabriel Chitupila ambae ni Mkuu wa Idara ya Kilimo na Mifugo Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma alipokuwa akitoa ufafanuzi wa mpango wa serikali kwa wafanyabiashara wa Mazao, Wamiliki wa Magala, Watendaji wa Vijiji Kata na Maafisa ugani amesema kwa sasa Wakulima hawatafuatwa Mashambani na wafanyabiashara bali watauza Mazao yao kwenye Vituo maalum

Wafanyabiashara watakuwa wananunua Mazao  kutoka kwa wakulima baada ya kufikishwa kwenye Vituo vilivyosajiliwa kisha wafanyabiashara wa ndani watakuwa wanawauzia wenzao kutoka nje ya nchi badala ya kwenda mashambani ambapo hatua hiyo imekataliwa na  baadhi ya wafanyabiashara kuwa italeta usumbufu kwa wakulima kwa madai watashindwa kutatua shida zao za dharula

Hofu hiyo ya Wafanyabiashara wa Mazao ya Kilimo imetafsiliwa kuwa watakosa namna ya kunufaisha zaidi kwa wengi wao wamekuwa wakiwafuata wakulima Mashambani na kujipangia bei wanayotaka huku wao wakiuza kwa bei za juu zaidi na sasa wanaelekea kukosa fursa hiyo

Akijibu Hoja hizo Gabriel Chitupila amesema katika maeneo mengi walipopita kufanya usajili wa wafanyabiashara na maghali walalamikaji ni Madalali na Wafanyabiashara badala ya Wakulima kwani kati yao hakuna anayemtetea Mkulima anaetumia garama kubwa na kipato chake ni kidogo na kueleza utaratibu wakulima hawatauzia Mazao Mashambani na hatua hii itawasaidia wafanyabiashara Wandani ya nchi hasa wapouza zao la Mhogo

Kuwafuata wakulima Mashambani ni kuwanyonya wakati wanatumia garama kubwa kwenye kilimo kwani ushawishiwa kuuza kilo moja ya Mhogo kwa Sh 100 hadi 150/badala y ash 800 na 1400 ambapo pia wafanyabiashara utumia nafasi hiyo kukwepa kulipa ushulu

Diocles Rutema Mkurugenzi Mtendaji amesema kumekuwepo na uholela katika Biashara za Mazao na kuikosesha mapato  Halmashauri ya Wilaya na kuwatoa hofu Wafanyabiashara kuwa suala hilo litatekelezeka kwa amani tena kwa mafanikio na kuongeza kuwa hayo ni maelekezo ya serikali nchi nzima na kueleza kuwa katika halmashauri ya kibondo wao wameshajipanga linalohitajika kila mmoja afuate taratibu zilizowekwa na kufuata maelekezo yatakayoendelea  kutolewa

''Kila mtu atatakiwa kusajili mazao yake ya Biashara anapoyaingiza kwenye Ghala na anapouza anatakiwa kuonyesha kwenye mfumo ili ifahamike aliingiza Mazao kiasi gani na yaliyotoka na kubaki ni kiasi gani''alisema Rutema

Mpaka sasa Wafanyaniashara wa wa Mazao waliokwisha sajiliwa kwenye mfumi wilayani Kibondo ni109,Wamiliki wa Maghala ni 171 Vituo vya kuuzia Mazao ni 38 na Vizuia ni 2 ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Aggrey Magwaza akieleza kuwa hatua hiyo itasaidia katika masuala ya ulinzi kwani Wafanyabiasha wengine kutoka Burundi, Rwanda na Congo DRC na Uganda uingia Mashambani kwa wakulima

Biashara ya Mhogo imekuwa ikishika kasi kila uchw




Baadhi ya washiriki waliohudhuria Kakikao kwa ajili ya kutoa na kupokea maelekezo ya serikali namna ya kununua na kuuza mazao ya Kilimo Kilichofanyika ukumbi wa Mikutano Mjini Kibondo Mkoani Kigoma

Kanali Aggrey Magwaza Mkuu wa Wilaya ya Kibondo alipokuwa akiwahutubia wafanyabiashara Mjini Kibondo

Diocles Rutema Mkurugenzi Mtendaji Hshauri ya Kibondo

Gabriel Chitupila Mkuu wa Idara ya Kilimo na Mifugo Hshauri ya Kibondo alipokuwa akitoa maelekezo kwa wafanyabiashara wa Mazao ya Kilimo

ao na kuonekana ni Bidhaa muhimu kwa wakazi wa Mkoa wa Kigoma hususa Wilaya za Kakonko Kibondo na Kasulu ambapo Wanunuzi wengi wamekuwa wakitoka nchi za ukanda wa Maziwa makuu hali ambayo imekuwa ikichangia kiunua maisha ya Watanzania 


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji