WATAALAM WA KILIMO TIMIZENI WAJIBU WENU
WATAALAM WA KILIMO TIMIZENI WAJIBU WENU
Kibondo. Wataalam wa Kilimo Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma wametakiwa kutimiza Wajibu wao kufanya kazi kwa weredi na uadilifu ili kuboresha sekta ya Kilimo
Wakulima wamekuwa wakikatishwa tamaa na mienedo ya baadhi ya Maafisa Ugani maeneo ya Vijijini kutokana na baadhi yao kutokuwa na kutowafikia Wakulima ili kuwaelekeza namna ya kuendesha shughuli za Kilimo na uzalishaji kuwa katika viawango visivyoridhisha
Akifunga mafunzo kwa Maafisa Ugani wa Halmashauri za Wilaya za Kasulu na Kibondo Mkuu wa Idara ya Kilimo na Mifugo Wilaya ya Kibondo Gabriel Chitupila akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Diokles Lutema jana aliwataka Maafisa Ugani hao kuwasaidia wakulima kwa hali na mali kwani wengi wamekuwa wakikosa ushauri wa kitaalam na kulazimika kuendesha kilimo isivyostaili
Chitupila aliongeza kuwa Mafunzo hayo ya siku tano kwa Maafisa ugani hao kwa ajili ya kuwajengea uwezo Maafisa ugani hivyo wayatumie vema kuwasaidia Wakulima namna kuandaa Mashamba Kupanda , Kuvuna hata kuhifadhi Mazao
Mafunzo hayo yaliandaliwa na Chama cha Wahitimu wa Chuo Kikuu cha KilimoSokoine Morogoro SUA SUGECO na kufadhiliwa na shirika la maendeleo la Umoja wa Mtaifa UNDP kupitia Mpango wa pamoja Mkoani Kigoma
‘’Kutokana na mchango wa UNDP SUGECO katika Sekta ya Kilimo Wilaya yangu inaahidi kushirikiana na SUGECO na UNDP katika kuhakikisha mafunzo haya yanaleta tija katika maeneo lengwa ya Mradi na maeneo mengine kwa ujumla ikikumbukwa kwa sasa Wananchi wa Kibondo wanategemea Kilimo cha Mhogo kibiashara’’alisema Chitupila
Erick Thomas ambaye ni Mkufunzi kutoka Chama cha Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo SUGECO alisema wameweza kutoa mafunzo kwa maafisa Ugani 7 kutoka Kibondo na watatu kutoka Kasulu na Waratibu wawili ili kujenga uelewa na ujuzi ambao watasaidia Wakulima 40 kila mmoja
Aidha amebainisha kuwa wamejifunza namna ya kukausha Mhogo kwa njia ya Teknolojia ya Umeme Jua yaani Solar ambao utasaidia kuandaa bidhaa bora kwa ajili ya ushindani wa Kibiashara kutokana na Mhogo unaokaushwa na jua kukosa ubora
Vile vile mradi huu unahusisha utoaji wa pembejeo bora kwa Wakulima ikiwemo mbegu bora za Mahindi ya Njano KG 3000 Maharage Kg 1000 Mbegu za Mhogo kwa eneo la Hekali 20 na Mbolea aidha Mradi kupitia watafanya Tathmini ya masoko kwenye Mnyororo wa thamani wa Mahindi,Mhogo na Maharage na kufunga Kaushio linalotumia mwanga wa Jua Solar dryer katika Halmashauri ya Kibondo ili kuwasadia wakulima kuongezea thamani Mazao yao
Nao baadhi ya Washiriki ambao ni Devotha Balenga na Mohamed Mambo wakitoa shukrani zao wameahidi kufanya kazi kwa mujibu wa taratibu na miongozo ya kazi ili kutoa mwelekea wa masuala ya kilimo kwa wakulima ili kufikia malengo yanayokusudiwa
Maoni
Chapisha Maoni