SEKTA BINAFSI KUSHIRIKISHWA UENDESHAJI RELI
SEKTA BINAFSI KUSHIRIKISHWA UENDESHAJI RELI
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Uchukuzi Prof.Godius Kahyrara amesema Serikali inaendelea kuboresha
miundombinu na sheria zinazosimamia usafiri wa reli Nchini ili kuruhusu sekta
binafsi kuendesha treni zao katika reli ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na ya
Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).
Prof. Kahyrara
ameyasema hayo jijini Dodoma wakati aliposaini mkataba wa Utendaji kazi kati
yake na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC)Masanja Kadogosa na
kusisitiza kuwa tija ya maboresho hayo ni pamoja na kukuza patola taifa na
urahisi kwenye usafirishaji wa mzigo kutoka eneo moja kwenda jingine.
“Shirika la TAZARA na
TRC ni miongoni mwa mashirikayanayopewa kipaumbele kwa sasa katika sekta ya
Uchukuzi na maeneo yanayotazamwa ni pamoja na uboreshaji wa miundombinu ambayo
kwa muda mrefu haikukarabatiwa” amesema Prof.
Kahyrara.
Katibu Mkuu Prof. Kahyrara amesema maboresho yanayofanywa katika
sekta ndogo ya reli yataongeza tija katika usafirishaji ikiwemo kupunguza
gharama za usafirishaji na hivyo kuruhusu bidhaa kuwafikia walaji kwa kwati na
kwa bei nafuu.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa TRC Bw. Masanja Kadogosa amesema miradi mbalimbali ya maboresho
katika reli ya kati inaendelea kutekelezwa ili kuirudisha katika ubora
unaotakiwa.
Mkurugenzi Kadogosa
ameongeza kuwa kwa reli ya Kisasa ya SGR ujenzi unaendelea na tayari baadhi ya
vitendea kazi kwa ajili ya uendeshaji vimeshawasili ikiwemokichwa kimoja cha
reli hiyo pamoja na mabehwa ambayo hivi karibuni majaribio yanatarajiwa kuanza.
Naye Mkurugenzi wa Tathimini na
Ufutiliaji kutoka Wizara ya Uchukuzi Bi. Devota Gabriel amemuhakikishia Katibu
Mkuu Prof. Kahyarara kuwa kitengo hichokimewekea mikakati thabiti
itakayowezesha wataalam wa Wizara kusimamia kwa karibu miradi iliyopangwa
kutekelezwa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ili kuzingatia thamani na ubora.
Maoni
Chapisha Maoni