KASEKENYA: TUMIENI WATAALAM ACHENI KUOGOPA GHARAMA

 





KASEKENYA: TUMIENI WATAALAM ACHENI KUOGOPA GHARAMA

 

Serikaliimetoawito kwa Mashirika, Taasisi za Serikali pamoja na Sekta Binafsi kushirikisha watalaam wa fani ya WabunifuMajengo katika utelelezaji wa miradi mbalimbali ya majengo, barabara namadarajailikuletaubunifu wa kipekee katika miji nakuifanyaiwe yenye mandhari bora.

 

Witohuoumetolewajijini Dar es Salaam naNaibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya, katika Mkutano wa 27 naKumbukizi ya Miaka 40 ya Chama cha WabunifuMajengo Tanzania (AAT), ambapo pamoja na mambo mengineamesisitizaelimuzaidiitolewekuhusuumuhimu wa tasniahiyo katika shughuli za ubunifu wa majengohasa kwa Sekta Binafsi.

 

“Nisemetu kama mtanzania wakati fulanihatutumiisanawataalamambaomwisho wa sikuutapatakaziyako nzuri, ya uhakikana yenye usalama kwa kuhofia gharama kubwanamatokeoyaketunaenda kwa watu wa barabaranibilakufahamuatharizakehivyoni jukumu lenukuwaeleshawananchikuhusufani hii”, amesema Eng. Kasekenya.

 

Kasekenyaameoneshaumuhimu wa Wataalamhaokuungana pamoja ilikushiriki katika miradimikubwanakujijengeauwezoilikuipunguzianchiutegemezi wa wataalamkutokanje wakati wa ujenzina matengenezo ya miundombinu ya barabara, madarajanamajengoambayoinajengwa kwa gharama kubwa.

 

AmewatakaWabunifuMajengowaliosajiliwanachamahicho kuwa wataalamwabobeziwatakaotoa huduma nzuri iliyo bora na kwa gharama nafuu kwa wananchi, Sekta Binafsi naSerikali.  

 

“HatutegemeiMbunifumajengoaliyesajiliwana AAT chini ya usimamiziwenukutoa huduma chini ya kiwangonaisiyokuwanamaadilimazuri”, amesisitiza Eng. Kasekenya.

 

Aidha, Kasekenyaamesema Wizara imechukuaombi la ushirikishwaji wa WabunifuMajengo katika usanifu wa barabara, madaraja, vituo vidogo vya mabasi, miundombinu ya njia za waenda kwa miguuilikupatamandhari nzuri ya miji  kwaupande wa miundombinu kama nchi za wenzetu.

 

Kwa upande wake, Msajili wa Bodi ya Usajili wa WabunifuMajengonaWakadiriajiMajenzi (AQRB), Arch. Edwin NnundumaamewatakaWabunifuMajengonchinikutafakari katika kipindi cha miaka 40 ya Chama hicho kama malengoyaoyametimiaikiwemo ya utoaji wa huduma bora ya majengo.

 

Arch. Nnundumaamekitaka Chama hichokujanamikakati ya kuijengatasniahiyo ya WabunifuMajengoikawe ya Ushindanindaninanje ya nchi.

 

“Bodiinategemea Chama hikikiendembelezaidi ya majukumu ya Bodinahasa katika kutoa huduma bora kwa umma, kubainimapungufuyaliyopo kwa wataalamnatasniayenyewenakuwasilishaSerikalini kwa lengo lakuongezaidadi ya wataalamweledinawenyeuzoefunakuwezakuaminiwazaidi katika uvumbuzi, usimamizinakutoamafunzo”, amefafanua Arch. Nnunduma. 

 

Naye, Rais wa Chama cha AAT, Arch. David Kibebe, ameishukuru Wizara ya Ujenzi kwa kushughulikia suala la kuandaasheria za ujenziambazo Chama imekuwa ikilizungumzia kwa kipindikirefu.

 

Arch. Kibebeameeleza kuwa Chama kwa kushirikiana naBodi ya Usajili wa WabunifuMajengonaWakadiriajiMajenziwamekuwakiungokikubwa katika kutoamafunzo kwa vijanawanaotarajiakusajiliwanabodihiyo kwa mujibu wa Sheria.

 

Chama cha WabunifuMajengo Tanzania (AAT), kiliundwa rasmi Mwaka 1982 ambapokilikuwanawanachamawasiozidi 15 ambapompakakimesajilijumla ya wanachama 1,200 kikiwanalengo la kuhakikishafanihiyoinaendelezwanainafanywa kwa welediilikutoa huduma bora kwa jamiinaSerikali.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji