Misri wavutiwa na miradi ya PPP ya TANROADS
Misri wavutiwa na miradi ya PPP ya TANROADS BALOZI wa Misri nchini Tanzania, Sherif Abdelhamid amevutiwa na miradi itayojengwa kwa ubia wa kati ya sekta binafsi na umma (PPP) itakayokuwa chini ya Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), imeelezwa. Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Mohamed Besta amesema hayo jana mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo na Balozi huyo yaliyofanyika Makao Makuu ya TANROADS jijini Dar es Salaam. Mha. Besta amesema Balozi huyo ameahidi kushiriki fursa zinazopatikana kwenye miradi ya TANROADS na ameonesha dhamira ya makampuni ya Misri kuja kushiriki kwenye miradi ya PPP, ikiwemo ya barabara ya kulipia ya kutoka Kibaha, Chalinze hadi Morogoro; na Barabara za Mzunguko za Jiji la Dar es Salaam (Dar es Salaam Outer Ring Roads). Miradi mingine ya PPP ni Daraja la Pili la Kigamboni; Barabara ya kulipia ya kutoka Morogoro hadi Dodoma na barabara ya kutoka Igawa hadi Tunduma. “Kama alivyosema hizi ni mojawapo ya fursa na u zoefu wa Kimatai...