PAC YAKAGUA MRADI WA UBORESHAJI KIWANJA CHA NDEGE TABORA
PAC YAKAGUA MRADI WA UBORESHAJI KIWANJA CHA NDEGE
TABORA
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imetembelea
na kukagua mradi wa ukarabati na uboreshaji wa Kiwanja cha ndege cha
Tabora unaotekelezwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).
Kamati hiyo ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Mheshimiwa
Japhet Hasunga (Mb), ikiwa mkoani Tabora Machi 17, 2024 imeshauri kwa
Wakala huo masuala mbalimbali ikiwemo kumsimamia Mkandarasi
kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huo ili wananchi wa Tabora na
mikoa jirani waweze kunfaika na mradi huo.
"Msimamieni Mkandarasi aongeze kasi ya utekezaji wa mradi ili ukamilike
kwa wakati, nao wananchi wa Tabora na mikoa jirani waweze kufurahia
huduma ya usafiri wa anga", amesema Hasunga.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Ludovick
Nduhiye amesema Wizara imepokea ushauri na maelekezo ya Kamati na
kuahidi kuyafanyia kazi kwa manufaa ya jamii na Taifa kwa ujumla.
Awali akiwasilisha taarifa ya mradi huo, Mtendaji Mkuu wa
TANROADS, Mhandisi Mohamed Besta amesema Mradi huo umefikia
asilimia 38 na unahusisha Ujenzi wa Jengo la abiria litakalohudumia abiria
120 kwa wakati mmoja, Mnara wa kuongoza ndege, barabara ya kuingia
na kutoka kiwanjani pamoja na ujenzi wa uzio wa usalama wenye urefu wa
kilometa 6.25
Mradi wa Uboreshaji na Ukarabati wa Kiwanja cha Ndege cha Tabora
utagharimu Tsh. Bil. 24 na unatarajiwa kukamilika tarehe 11 Oktoba 2024.
Maoni
Chapisha Maoni