DHAMIRA YA SERIKALI NI KUKUZA UCHUMI WA SEKTA BINAFSI KWA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI: BASHUNGWA






 DHAMIRA YA SERIKALI NI KUKUZA UCHUMI WA SEKTA BINAFSI KWA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI: BASHUNGWA

Waziri wa Ujenzi naMbunge wa jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwaameeleza kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sitanikukuzauchumi wa Sekta binafsi inayochangiamakusanyo ya kodiambazozitawezeshaujenzi wa miundombinu ya barabara nautekelezaji wa miradimingine ya maendeleonchini.

Bashungwaamezungumza hayo Machi 27, 2024 katika kikaokilichowakutanishawafanyabiashara wa Wilaya ya Karagwe pamoja naTaasisi za Serikalizinazowahudumiaambapoamesikilizakerozaoikiwemotozokubwa za kodi, ushuru pamoja nakaulizisizoridhishakutoka kwa Maafisa wa Mamlaka ya Mapato (TRA).

Bashungwaamesisitiza kuwa ukusanyaji wa mapatounawezeshaSerikalikufanikishamalengoyake ya kuhudumianchi pamoja nawananchi wake kwa haraka kwa kuwa wajibu wa Serikalinikujengaustawi wa wafanyabiasharana sio kuwadumaza.

“Sijafurahishwanamadai ya kauli za Maafisa kwa wafanyabiasharaambazo sio sahihi,kwakuwaaambiawakishindwakulipakodi,  wafungebaishara, Lengo la Serikali ya Rais, Dkt. SamiaSuluhu Hassan kuwawezesha kwa kutoaelimu, kuwashaurinakustawishawafanyabiashara” amesisitizaBashungwa.

Aidha, Bashungwaameutaka uongozi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Kagera kusimamia miongozo pamoja nakutoaelimu ya Sheria na Kanuni za kodimara kwa mara kwa wafanyabiashara pamoja naMaafisakuwa nakauli nzuri nawezeshi.

BashungwaamelitakaBaraza la wafanyabiashara la Wilaya ya Karagwekutimizawajibuwao kwa kuitishamikutano ya mara kwa maranawafanyabiasharawoteilikukumbushanamasualatozo mbalimbali zilizoponakutatuachangamotozao kwa kuzipatiasuluhu ya harakakablamfanyabiasharahajafikia hatua ya kufungabiashara.

Kuhusuutekelezaji wa miundombinu, BashungwaamesemaSerikaliinaendeleanautekelezaji wa barabara ya Bugene-Benaco (km 128.5) pamoja nakuanzautekelezaji wa barabara ya Omurushaka - Kyerwa (km 50) naOmugakorongo – Kigarama -  Murongo (Km 111) kwa kiwango cha lami.

Naye, Mfanyabiashara wa Kampuniya SANOA, Bw. MetiselaPhilipoameeleza kuwa kodinafainiwanazotozwazimekuwakubwanahaziendaninabiasharawanazozifanyahivyokupelekeabaadhi ya wafanyabiasharakufungabiasharazao.

Kwa upande wake, KaimuMeneja wa TRA Mkoa wa Kagera, Bw. OmaryKigodaamesema kuwa suala la lughambaya kwa walipakodi sio msimamo wa Taasisihivyo TRA itaendeleakuwachukulia hatua baadhi ya watumishi ambaowanaendakinyumenamaadili ya utumishi.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Karagwe, Paschal Rwamugataamesema kuwa moja ya majukumu ya Chama nikusikilizakero za wananchinakuitakaSerikalikutatuakerohizo kama ambavyo imekuwa ikifanya

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao